Sunday 30 April 2017

#BREAKING NEWS>>>Tetemeko jingine latokea Bukoba.

Reporter wa AyoTV ameripoti kutokea mtaa wa Rwamishenye manispaa ya Bukoba kwamba limetokea tetemeko. Amesema tetemeko hilo ambalo limetokea mida ya saa saba na nusu usiku huu wa kuamkia April 30, lilidumu kwa sekunde zisizozidi 15.

Mpaka sasa anazunguka kwenye mitaa mbalimbali na anachoshuhudia ni Watu mbalimbali waliotoka nje ya nyumba zao kuhofia tetemeko jingine. Hakuna madhara yoyote yaliyoripotiwa mpaka sasa lakini AyoTV na millardayo.com zinaendelea kufatilia kwa ukaribu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment