Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alisimama mbele ya bunge na kuomba msamaha
ikiwa ni wiki kadhaa tangu atuhumiwe kosa la kutumia lugha cha chafu kwa
Spika wa Bunge, Job Ndugai.
“Mwenyekiti tarehe nne mwezi wa nne wakati wa uchaguzi wa Iyala kuna
matuklio ambayo yalitokea yakanipelekea kuzungumza lugha ambayo
kitamaduni za Bunge sio sawa na lugha husika ilimgusa muheshimiwa spika
na muheshimiwa Kigwangalla kwa namna moja au nyingine kama mbunge mzoefu
nilitumia kuzungumza na kuomba radhi wahusika katika individual
capacity lakini vilevile nikaona ni busara kwasababu haya maneno
nilizungumza bungeni lakini pia kuzungumza na kumuomba radhi Muheshimiwa
Spika kwahiyo niliomba huu muda specifically kumuomba radhi kumuambia
namheshimu na kumwambia sitarudia, spika ni kiongozi wangu lakini pia ni
mwananchi wa jimbo la Kawe,” aliomba radhi Mdee.“Kwahiyo nina kila sababu yakuyazingatia haya mawili kwa umakini mkubwa kwahiyo ninaomba radhi kwake ninaomba radhi kwa Kigwangalla ninaomba radhi wka Bunge, ninaomba radhi kwa wananchi wa bunge la Kawe ambao miongoni mwenu nyie ni miongoni mwa wananchi wa jimbo la Kawe na niwaaahidi tu kuna baadhi ya wananchi Watanzania ntakuwa nimewakawanza kwahiyo ninaomba radhi niaahidi tu michango yangu ya bunge itaendelea kama kawaida lakini kwa kutumia lugha za staha.”
Mbunge huyo alitoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment