Wanaume wanaougua maradhi ya kisukari huweza kuwa katika hatari kubwa ya
kukubwa na upungufu wa nguvu za kiume kuliko wanaume wasio na maradhi
hayo.
Inapotokea sukari haikudhibitiwa katika damu huweza kusababisha
kuharibika kwa neva na misuli midogo inayodhibiti kusimama kwa uume.
Hata hivyo, mbali na sababu hizo za magonjwa pia kuna sababu nyingine za
kibinadamu ambazo huweza kuchangia tatizo hilo la upungufu wa nguvu za
kiume ikiwemo hizi zifuatazo ambazo huchangiwa na wanawake.
Usafi kwa mwanamke:
Hali ya usafi ni muhimu hasa zile sehemu muhimu ambazo huusika kwenye
tendo la ndoa endapo mwanamke atakuwa si msafi basi huweza kumsababishia
mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.
Naamini kwamba kila mtu hupenda usafi na wengi wetu tunafahamu kero za
uchafu wakati wa tendo, kwa mantiki hiyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa
mchafu huweza kusababisha mwanaume kupoteze msisimko na uwezo wa tendo
la ndoa.
Mwanamke kuwa msafi ni muhimu sana, kuanzia mavazi na mwili pia hii itasaidia kuleta msisimko zaidi katika mapenzi.
Kutokuwa na uhodari na ujuzi
Wanawake wengi huhofia sana kuonesha ujuzi wao wa kimapenzi wanapokuwa
na wapenzi wao, huku wengi wakiogopa kuhisiwa huenda ni wazoefu zaidi
katika masuala hayo ya kimapenzi, lakini si kweli ujuzi na uhodari kwa
mwanamke ni muhimu zaidi kwani huleta hamasa kwa mwanaume na hivyo
kumsaidia kuepukana na shida ya upungufu wa nguvu za kiume.
Tatizo hili lipo zaidi kwa wanawake ambao tayari wapo ndani ya ndoa,
wengi wao huwa hawajishughulishi kumsaidia mwanaume kupata mihemko zaidi
na wala hawana ubunifu jambo ambalo humfanya mwanaume kushiriki tendo
kwa kutegemea hisia zake mwenyewe pekee, hali ambayo si nzuri kwani
mwanaume ikitokea atakuwa na mawazo au kuchoka hatoweza kupata mhemko
kwasababu hapati ushirikiano toka kwa mwenzake (mwamke).
Karaha za maneno
Pale inapotokea mwanamke akawa ni mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na
matusi basi hali hiyo huweza kumfanya mume amchukie na kutopenda
kushiriki naye tendo. Jambo ambalo baadaye husababisha wanaume wengi
kuanza kutoka nje ya ndoa zao.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment