Simba Sports Club
D'salaam, Tanzania
22/4/2017.
TAARIFA KWA UMMA
Klabu
Ya Simba SC inapenda kuwajulisha wanachama na wapenzi wake kuwa
imesitisha maandamano iliyopanga kuyafanya Jumanne wiki ijayo 25.04.2017
, baada ya nia na dhamira njema ya serikali kutaka kushughulikia
sintofahamu inayoendelea baina ya klabu na Shirikisho la Soka nchi
(TFF).
Ikumbukwe
jana klabu yetu , ililiandikia barua Jeshi la Polisi nchini ikiomba
kibali cha maandamano ya amani, yaliyopangwa kuhudhuriwa na
viongozi,wanachama na washabiki wa klabu yetu kwenda Wizara inayosimamia
Michezo nchini, yakiwa na lengo la kupeleleka kilio chetu juu ya namna
TFF inavyoshughulikia malalamiko ya muda mrefu na ya sasa ya klabu
hii kubwa nchini.
Katika
barua iliyoandikwa na katibu Mkuu wa Baraza la michezo nchini (BMT)
Mohammed Kiganja kwa niaba ya Serikali, imetutaka Shirikisho na Klabu
kutafuta namna sahihi na iliyo na weledi katika kushughulikia changamoto
hizi zinazoweza kuvuruga amani ya nchi.
Serikali
kupitia barua hiyo,imeahidi pia kutukutanisha pande zote haraka
iwezekanavyo,ili kwa pamoja tumalize sintofahamu hii kwa maslahi ya
mchezo wa mpira wa miguu Tanzania.
Klabu
ya Simba inachukua nafasi hii ya kipekee kuishukuru serekali kupitia
baraza la michezo la taifa ( BMT) kwa hatua mahsusi na za haraka katika
kutafuta suluhisho la kudumu la jambo hili.
Tunawaomba
wanachama na washabiki wetu watulie na sote tuache majibizano yoyote
ili kutoa fursa kwa Serikali kusimamia kikamilifu jambo hili.
Klabu ya Simba inafanya mawasiliano na Jeshi la Polisi nchini kuwajulisha kusudio letu la kusitisha maandamano hayo.
IMETOLEWA NA...
Haji S Manara
Mkuu wa Habari wa Simba Sc
Simba nguvu moja
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment