Labda ulikuwa miongoni mwa watu waliosikia taarifa ya kukamatwa kwa
muuza madawa ya kulevya nchini Mexico, JoaquÃn Guzmán Loera AKA “El
Chapo Guzmán”, na ukajiuliza kuhusu wauzaji madawa ya kulevya ambao
waliwahi kutokea katika dunia hii.
Wapo wengi ambao walikuwa wauzaji wa madawa ya kulevya, mabilionea
ambao mwisho wao ulikuwa mbaya kama Pablo Escobar. Kama ulikuwa huwajui,
hii hapa chini ni orodha ya wauzaji madawa ya kulevya hatari ambao
wamewahi kuwepo katika dunia hii mpaka sasa.
Mwaka 1975, jamaa alivamiwa nyumbani kwake, ndani ya nyumba tu
kukakutwa kiasi cha dola laki tano (zaidi ya bilioni moja), kwa kipindi
hicho, kilikuwa kiasi kikubwa sana cha fedha. Jamaa alipokamatwa,
akafungwa gerezani miaka 75 kwa kesi zaidi ya 100 za madawa ya kulevya.
FRANK LUCAS AKA Superfly
Unapowazungumzia wauza madawa ya kulevya ambao wamewahi kuishi
katika hii dunia basi hutoweza kuliacha jina la mshikaji huyu,
Mmarekani, ‘bitozi’, bilionea ambaye utajiri wake mkubwa ulitokana na
uuzaji wa madawa ya kulevya.
Jamaa alivuma sana miaka ya mwishoni mwa mwaka 1960 na mwanzoni mwa
mwaka 1970. Jamaa alikuwa na washikaji wengi waliokuwa wakipiga
biashara hii haramu. Kila siku, alisafirisha madawa ya kulevya kupitia
kwenye majeneza ya watu aliokuwa akiwaua na washikaji zake.
CHRISTOPHER COKE AKA: “Dudus”
Jamaa alikuwa mpiga dili mkubwa tu kwenye biashara ya madawa ya
kulevya. Alikuwa Mjamaika, mwenye sura ya kipole, kusaidia watu ambapo
baada ya kugundulika kwamba anafanya biashara hiyo, hakutaka hata
kutafutwa, mwenyewe akajipeleka polisi mwaka 2010.
Mshikaji aliingiza kiasi kikubwa cha fedha, mpaka kukamatwa kwake
alikuwa ameingiza kiasi cha dola bilioni 30 (zaidi ya trilioni 60)
ambapo kwa sasa tungesema kwamba yeye ni tajiri wa 18 duniani.
Japokuwa alikuwa na ubaya wake wa kufanya biashara hiyo haramu
lakini mshikaji alikuwa mtu wa watu. Alikuwa akijenga hospitali, kufanya
biashara nyingine na kuwaajiri watu wengi, aliwasaidia masikini na
kuwafurahisha kwa kuyaboresha mazingira yao japokuwa upande wa nyuma,
aliteketeza vijana kwa kuwauzia biashara hiyo.
Mwaka 2004 akatolewa gerezani lakini ilipofika mwaka 2012, akauawa
kwa kupigwa risasi na mshikaji aliyekuwa akiendesha pikipiki. Huo ukawa
mwisho wake, akazikwa ingawa bado anajulikana kama mfanyabiashara mkubwa
wa biashara hiyo haramu.
Jamaa alianza kufanya biashara hiyo miaka ya 1980. Alianza kama
‘punda’ yaani mbebaji lakini baadaye akajizatiti na kuwa na biashara
yake mwenyewe. Jamaa alikuwa akiuza mzigo wa dola milioni 3 (zaidi ya
bilioni 6) kila siku iendayo kwa Mungu. Mshikaji alikuwa akiuza kilo 400
kila wiki.
GRISELDA BLANCO AKA: “The Cocaine Godmother”
Unaweza kumchukulia poa tu kwa sababu ni mwanamke lakini ni lazima
ujue kwamba kwa watu waliokuwa wakifanya biashara ya kulevya kwa kiasi
kikubwa huwezi kumuacha huyu mwanamke.
Alikuwa mtu wa dili, mbali na uuzaji wa madawa hayo, pia alikuwa
muuaji mzuri tu ambaye kwa kipindi chote cha kufanya biashara yake,
aliwaua watu 200 kwa risasi, tena kwa mkono wake mwenyewe.
Baada ya kufanya biashara hiyo kwa miaka kadhaa, akakamatwa na
kufungwa miaka 20 gerezani, ila cha kushangaza sasa, akiwa hukohuko
nyuma ya nondo, michongo yake ya biashara ilikuwa ikisonga kama kawa.
Rick Ross AKA: “Freeway”
Siyo huyu unayemjua wewe! Siyo yule jamaa mwenye mwili mkubwa,
mwanamuziki wa Kimarekani, achana na huyo, mshikaji mwenyewe alilichukua
jina la Rick Ross kutoka kwa huyu jamaa.
Mwili mdogo, mtanashati, alipenda kutabasamu lakini nyuma ya
tabasamu lake, jamaa alikuwa ‘mbaya’ kwenye biashara ya madawa ya
kulevya.
Arturo Beltrán Leyva AKA: “Boss of Bosses”
Kama washikaji wa hapo juu, hata huyu mwana alikuwa nuksi kwenye
uuzaji wa madawa ya kulevya. Mshikaji alikuwa na kundi lake liitwalo
Beltran Leyva Cartel, kundi lililosumbua sana nchini Mexico.
Kulikuwa na kesi nyingi dhidi ya kundi hilo, watu walikuwa
wakiuawa, wanawake walibakwa, walisafirisha sana silaha kwenda sehemu
mbalimbali, wengine waliteswa na kutekwa. Kwa kifupi, kundi hili
lilikuwa hatari zaidi kuliko makundi mengine yaliyowahi kutokea huko.
Jamaa aliuawa na wanajeshi wa majini mwaka 2009 katika majibizano ya kurushiana risasi na wanajeshi hao.
Alipokamatwa, alifungwa jela miaka mingi tu ila wakati akiwa
ametumikia kifungo kwa miaka miwili, kuna jamaa hukohuko jela akamuua
kwa kumchoma kisu, hiyo ilikuwa mwaka 1986 na mazishi yake yalihudhuriwa
na watu wengi, sawa na mazishi ya aliyekuwa mwanaharakati, Martin
Luther King Jr.
Felix Mitchell AKA: “The Cat”
Jamaa alikuwa si kitoto, huyu ni miongoni mwa wauza madawa ya
kulevya wakubwa waliowahi kutokea duniani. Alikuwa na kundi lake
liitwalo 69 Mob. Jamaa alikuwa akipiga dili za chinichini, ilikuwa
vigumu kukamatwa kwani alikuwa mjanja kupindukia.
Amado Carrillo Fuentes AKA: “Lord of the Skies”
Alikuwa Mmexico aliyekuwa akifanya biashara ya madawa ya kulevya
kwa kiasi kikubwa. Hakuwa mkuu wa kitengo, aliajiriwa na bosi wake
aliyeitwa Rafael Aguilar Guajardo ila akaamua kumuua na kushikilia yeye
hicho kitengo.
Ndiye muuzaji pekee wa madawa ya kulevya aliyekuwa akiingiza kiasi kikubwa nchini Marekani kuliko mtu yeyote.
Alikuwa bilionea, mwenye kupenda watu na kusaidia masikini. Hakuwa
na utani katika biashara hiyo, aliua wote aliohisi kwamba walikuwa watu
wabaya katika biashara yake.
Alitumia ndege zake kusafirisha madawa ya kulevya kwenda nchini
Marekani mara nne kwa siku. Kumkamata haikuwa kazi nyepesi kwa sababu
alikuwa akibadilisha sura yake kwa kuvaa sura ya bandia.
Mwaka 1997 alipokuwa akifanyiwa upasuaji wa kuwekewa sura ya bandia
katika Hospitali ya Santa Monica nchini Mexico, dawa zilizidi hivyo
kufariki dunia na baada ya siku mbili, wale madaktari waliofanya
upasuaji huo wa kumuwekea sura ya bandia wakakutwa wameuawa kinyama na
miili yao kutupwa.
Pablo Escobar AKA: “The World’s Greatest Outlaw”
Huyu jamaa alikuwa kiboko, ni Mcolombia aliyekuwa akiuza madawa ya
kulevya kwa kiasi kikubwa. Alikuwa katili, kuua watu waliokuwa kinyume
naye ilikuwa ishu ndogo sana kwake.
Hakutaka mchezo, hakuwahi kuweka fedha benki, alikuwa akizihifadhi
ndani na wakati mwingine zilikuwa zikiliwa na panya. Kuna kipindi mtoto
wake alikuwa akiumwa, alizitumia dola za Kimarekani kumuwashia moto, eti
kupoza baridi lililokuwa likimpiga, kitu kilichowakasirisha sana
Wamarekani, waliona wamedharauliwa sana mpaka noti yao kuchomwa moto.
Alikuwa na utajiri mkubwa na mwaka 1989 alitangazwa kama tajiri wa
saba duniani akiwa na utajiri wa dola bilioni 25 (zaidi ya shilingi
trilioni 50). Jamaa alikuwa akimiliki 4/5 ya soko kubwa la madawa ya
kulevya duniani.
Jamaa alikuwa akisafirisha tani 15 za madawa ya kulevya kila siku
barani America. Jamaa aliua majaji 30 waliokuwa wakisimamia kesi zake na
polisi 400 ambao walionekana kimbelembele kumfuatilia kwenye mishe zake
na pia aliilipua ndege aina ya Avianca Flight 203 ambayo ilikuwa
ikimbeba waziri mkuu wa kipindi hicho nchini Colombia.
Kwa kifupi, jamaa alikuwa na pesa ndefu kiasi cha kuiambia serikali
yake kwamba imuache afanye mishe zake kwani angelipia deni la dola
bilioni 20 (zaidi trilioni 40) lililokuwa ikidaiwa, ila serikali
ikakaata na kumuua.
JoaquÃn Guzmán Loera AKA “El Chapo Guzmán”
Hapa ndipo kwenye kazi sasa. Huyu anaonekana kama mwamba wa
biashara hii ya madawa ya kulevya. Ni Mmexico mwenye mkwanja mrefu
ambapo amekuwa akiupata kupitia biashara yake haramu.
Alikuwa mtu anayetafutwa kwa nguvu zote kabla ya kukamatwa.
Aliwekeza nguvu kubwa katika biashara hii, Wamarekani na Wamexico
walimtafuta lakini hawakumpata.
Wakati wakiwa na uchungu naye, wakafanikiwa kumpata na hivyo
kufungwa nchini Mexico. Kutokana na fedha alizokuwa nazo, inasemekana
kwamba aliwahonga askari magereza na kutoroka kwa kupitia katika bomba
la choo, unaamini hilo?
Wamarekani walikasirika sana, wakaahidi kumtafuta, kweli wakaingia
mzigoni. Hawakuchukua muda sana, wakamnasa na hivyo kuiambia Serikali ya
Mexico kwamba watamfunga wao wenyewe ili wamuonyeshee kwamba wao si
watu wa mchezo, kweli wakamfunga na mpaka leo hii yupo gerezani
akiendelea kutumikia kifungo chake ambacho hakikuwekwa wazi ni cha muda
gani.
0 comments:
Post a Comment