Msanii wa filamu, Wastara Juma ameweka wazi sababu kubwa ambayo
ilimpelekea kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Bondi Bin Salim na kwenda
kuolewa na Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma kisha kuachana
naye na kurudiana tena na mpenzi wake
Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live cha (EATV) Wastara anasema
aliamua kuachana na Bond kutokana na tabia yake ya matumizi ya dawa za
kulevya aina ya mirungi na pombe pamoja na tabia zingine ambazo yeye
alishindwa kuvumilia na kuamua kuachana naye.
"Ukweli ni kwamba kuna issue nzito ilitokea kati ya mimi na Bond mpka
Bond mwenyewe aliamua kutoa ushuhuda na kutubu juu ya matumizi ya dawa
za kulevya aina ya mirungi, mpka aliamua kuondoka mwenyewe kwenda mbali
na mazigira ambayo mimi nilikuwa naishi, alikuwa anatafuta njia ya
kujisaidia ili aache vile vitu ambavyo binafsi nilikuwa sivipendi,
kwanza kwenye mahusiano kulikua hakuna uaminifu kabisa, ilifikia hatua
mpka kuna watoto wengi sana walikuwa wanaletwa wengine ni kweli wengine
wa uongo vile vitu binafsi kama mwanamke vilikuwa vinaniumiza" alisema
Wastara
Mbali na hilo Wastara anasema baada ya hapo familia yake ilimshawishi
aweze kuolewa na Mbunge huyo Sadifu ambaye alikuwa anahitaji kuwa naye
na kusema aliwasikiliza sababu siku zote familia yake huwa inaiweka
mbele na kuwasikiliza na kuamua kwenda kuolewa na Mbuge lakini anasema
baada ya kuingia huko alikutana na matatizo mara kumi ya alipotoka hivyo
ndoa hiyo ilimshinda ndani ya siku sabini na kitu na kuamua kuachana
naye.
Wastara alizidi kuelezea kuwa baada ya hapo Bond alirudi toka reharb
akiwa ameachana na tabia zake zile na alijiridhisha kuwa sasa
amebadilika hivyo akarudiana naye na wanaendelea kuishi pamoja mpka sasa
kama wapenzi.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment