Kiongozi
wa kanisa katoliki anayewasaidia raia wa Malta amejiuzulu kufuatia
mgogoro na Vatican kuhusu mpango wa kusambaza mipira ya kondomu
kulingana na kanisa hilo.
Mathew Festing mwenye umri wa miaka 67 alijiuzulu baada ya papa Francis kumtaka kufanya hivyo katika mkutano siku ya Alhamisi.
Hatua
hiyo inafuatia ufichuzi kwamba tawi la hisani la kanisa hilo huko Malta
lilisambaza maelfu ya mipira ya kondomu katika taifa la Myanmar.
Kanisa
katoliki linakataza utumizi wa mipira ya kondomu. Papa Francis alimtaka
ajiuzulu na alikubali. Tawi hilo la Malta lina uwezo mwingi kama ule wa
taifa zima. Hutoa pasipoti, stampu na leseni na pia lina uhusiano wa
kidiplomasia na mataifa 106 ,ikiwemo Vatican.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment