Miezi
takribani mitano iliyopita tangu aondolewe Billcanas, siku moja tangu
Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo katika shamba lake,
Mwenyekiti huyo wa Chadema amepewa siku 14 awe amelipa kodi
inayokadiriwa kufika milioni 13.5, ya hoteli yake ya Aishi iliyoko
Machame Mkoani Kilimanjaro.
Uamuzi
huo mpya wa Serikali wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro,umefikia
hatua hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Gellasius
Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la
Veggies analomiliki Mbowe kutokana na kile kilichosema lipo ndani ya
chanzo cha maji.
Byakanwa
amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano imelenga kukusanya mapato ili
iweze kutekeleza majukumu yake ikiwamo kutekeleza ilani ya Chama cha
Mapinduzi (CCM).
“Hatuwezi
kufikia malengo ya ukusanyaji mapato yetu ya ndani kama kuna
wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na tena kwa
kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo yataweza
kujulikana kiasi anachostahili kulipa kodi,”amesema Byakanwa.
Hata
hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amemshutumu Mbowe kwa kufanya uharibifu wa
mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha mkuu wa Wilaya
kulingana na uamuzi wa Kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta
maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa
maji mfereji.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment