Rais John Magufuli amemteua Anne Kilango Malecela kuwa mbunge, huku
akiwa mkuu wa mkoa pekee kwenye utawala wa awamu ya tano aliyedumu na
wadhifa huo kwa muda mfupi wa siku 29.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Rais Ikulu, imeeleza kuwa Kilango ataapishwa kwa mujibu wa taratibu za Bunge.
Uteuzi huu unakuja siku chache kabla ya Rais Magufuli kumteua aliyekuwa
mbunge wa kuteuliwa ambaye pia alikuwa Naibu Waziri wa Kazi, Dk
Abdallah Possi kuwa balozi. Tayari, Dk Possi amekabishi barua ya
kujiuzulu ubunge.
Hata hivyo, Kilango anarudi katika ulingo wa siasa huku akiwa amepitia
katika misukusuko kadhaa ikiwamo kupoteza kiti cha ubunge Same
Mashariki, mkoani Kilimanjaro.
Kilango aliteuliwa Machi 13, 2016 na uteuzi wake kutenguliwa Aprili 11
mwaka huohuo, kutokana na kutoa taarifa kwamba Mkoa wa Shinyanga
aliokuwa akiuongoza haukuwa na watumishi hewa.
Safari yake ya kisiasa
Mbunge huyo mteule alizaliwa Januari 9, 1956 Wilaya ya Same mkoani
Kilimanjaro. Mwaka 1979-1983 alikuwa mwalimu Sekondari ya Kisutu jijini
Dar es Salaam; 1983-1991 alikuwa Mhasibu Msaidizi Shirika la Ndege
Tanzania (ATC); na 1991-1993 alikuwa Mdhibiti wa Fedha Shirika la Ndege
la Gulf.
Pia, mwaka 1993-1994 alikuwa Mhasibu Shirika la Ndege la KLM; 1994-2000
alikuwa akijishughulisha na ujasiriamali kwenye kampuni yake ijulikanayo
kama Ninna Bridal Centre; 2000-2005 aliteuliwa ubunge na Rais Benjamin
Mkapa; na 2005-2015 alikuwa mbunge wa kuchaguliwa Same Mashariki.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment