Saturday 21 January 2017

Spika Ndugai Apokea Barua ya Kujiuzulu Ubunge ya Dk Abdallah Possi Aliyeteuliwa Kuwa Balozi..!!!..Fahamu zaidi hapa.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Job Ndugai amepokea barua ya kujiuzulu Ubunge iliyowasilishwa kwake na Dokta Abdallah Saleh Possi aliyeteuliwa kuwa Balozi katika kituo atakachopangiwa hapo baadae.

Taarifa ya Spika Ndugai ya kuwaarifu wabunge wote na wananchi kwa ujumla iliyotolewa jana imesema barua hiyo ya kujiuzulu Ubunge wa Dokta Possi imezingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 67(1) (g) ikisomwa pamoja na ibara ya 149 (1) (d), hivyo Spika wa Bunge amemwandikia rasmi Rais kuwa hivi sasa wabunge wa kuteuliwa na Rais waliopo Bungeni ni saba (7) na hivyo nafasi zilizowazi ni tatu (3) baada ya Dk Possi kujiuzulu.

Taarifa hiyo imetolewa na kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ofisi ya Bunge.


Download  Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi


Bonyeza Hapa CLICK HERE

                              Follow me instagram 

 

0 comments:

Post a Comment