Kocha
George Lwandamina amewata wachezaji wake kuondoa presha ya kuwaza
kurejea kileleni na badala yake wacheze kwa lengo la kuishinda Mwadui
FC, leo.
Yanga inakutana na Mwadui FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Iwapo Yanga itashinda, basi itapaa hadi kileleni ikiwa na pointi 46 na kuiacha Simba yenye 45 kileleni hadi sasa.
Simba imebaki pengo la pointi mbili tu kati yake na Yanga baada ya jana kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC.
“Kocha
kasisitiza suala la pointi tatu na si kuwenda kileleni. Ametuambia
tunachotakiwa kufanya ni ushindi kwa lengo la kupata pointi tatu.
“Ametukataza
suala la kufikiria kukaa kileleni kwa kuwa linaweza kutupa presha na
kushindwa kufanya vizuri dhidi ya Mwadui FC,” alisema mmoja wa wachezaji
wa Yanga ambaye sasa ni tegemeo.
Imeelezwa
Lwandamina anayesifika kwa uwezo mkubwa wa masuala ya saikolojia kwa
wachezaji amegundua kuna presha kubwa ya wachezaji kuhusiana na kukaa
kileleni na kuipita Simba.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment