Sayansi ya Teknolojia ikiwa inaendelea
kushika kasi siku hadi siku, chumba hiki maalum kilichojengwa juu ya
safu za milima ya Alpine iliyopo Ufaransa kimepata kuwa kivutio kikubwa
kwa watalii wanaotokea sehemu mbalimbali Duniani kutokana na staili ya
aina yake walivyokitengeneza kwa kutumia vioo vilivyozunguka kichumba
hicho kidogo hivyo kumuwezesha mtalii kuona kama vile yupo juu ya Dunia.
Unaambiwa sio rahisi kwa mtu mwenye roho nyepesi kuweza kusimama kwenye kichumba hicho kidogo kutokana na kuwa kileleni mwa mlima Alpine takribani umbali wa mita 3800 kutoka usawa wa bahari ambapo utengenezaji wake ulichukua takribani muda wa miaka miwili na ada ya kutembelea kwenye kivutio hicho ni kiasi cha Euro 55 ambazo ni sawa na Tsh 80,000 bila chenji (NADHANI WATAKUULIZA BARUA KUONESHA UMEAGA KWENU)
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment