USIKU wa Jumanne ya Aprili 15, 2012 vijana wawili wachezaji wa soka
wanabishana kuhusu kuondoka mahali walipokuwa ili wakapumzishe miili
yao baada ya pirika za kutwa nzima. Hao ni viungo wa soka, Ramadhan
Chombo ‘Redondo’ na Patrick Tabu Mutesa aliyekuwa maarufu kama Patrick
Mutesa Mafisango ambaye kwa sasa ni marehemu.
Wachezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa Mafisango.
KIONGOZI SIMBA ATOA FEDHA
Asubuhi ya Jumatano Apri- l i 16, 2012 akiwa ny- umbani kwake
Chang’ombe jijini Dar es Salaam, Mafi sango aliletewa fedha na kiongozi
mmoja wa Simba kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Baada ya kupokea fedha
hizo, Mafisango akiwa na Redondo alianza kulazimisha waanze kupata ‘moja
moto moja baridi’ lakini mwenzake alikataa hadi watakapopata chakula cha
mchana.
“Alionekana kutaka kinywaji sana lakini nilimsihi kwamba si vizuri
kutumia kinywaji muda huo badala yake asubiri hadi tutakapopata chakula
cha mchana kwanza,” anasema Chombo. Baadaye Mafi sango aliletewa gari
Toyota Chaser GX 100 kwa ajili ya kulitumia siku hiyo, lakini mpwa wake
Orly Ilemba na Ally Hassan ‘Bozy’ walitoka na gari hilo kwenda Magomeni.
Baada ya kuwasubiri kwa muda mrefu, Mafi sango na Redondo waliamua
kuwafuata Magomeni akina Orly baada ya kuona wanachelewa kurejea
Chang’ombe na gari hilo.
Kabla ya kula Mafi sango aliwarushia maneno akina Orly ambao
hawakuonyesha hamu ya kula chakula hasa baada ya kuwasema kwa kuchelewa
kuwafuata Chang’ombe.
AGAWA FEDHA NA KUAGA
Lari lakebaada ya ajali.
MAFISANGO APIGA USINGIZI WA AJABU
Walipofi ka Magomeni, Mafi sango na Redondo waliungana na akina Orly
kisha wakalekea Kinondoni ambako walipata chakula lakini jambo la
kushangaza baada ya kula, Mafi sango alilala usingizi mzito.
“Wakati
analala nikawaambia watu tuliokuwa nao kwamba wamuache apumzike na
alilala usingizi mzito sana hadi alipozinduka baada ya kama saa mbili
hivi,” anasema.
Karibu muda mwingi wa mchana, Mafi sango alikuwa akitoa fedha au
vinywaji kwa watu huku akisema kwa utani, kunyweni hamjui labda ndiyo
tunaagana au maisha haya mafupi sana. Hata fedha alikuwa akitoa kwa
baadhi ya watu aliokuwa akifahamiana nao na karibu wote alikuwa akiwapa
na kuwaambia maneno hayo.
“Sisi tuliona kama kitu cha kawaida lakini kumbe yeye sijui kuna
kitu alihisi au la, lakini alikuwa akitoa fedha na kutamka maneno ya
kuaga,” anasema Bozy.
SAFARI YA MAISHA CLUB
Mafisango alikuwa na asili ya DR Congo licha ya kuwa na uraia wa
Rwanda, alihamia Rwanda akiwa mkubwa na ni katika harakati za maisha ya
soka tu. Huko ndiko alikopata jina la Mafi sango ambalo ni la ukoo wa
mwanamke aliyezaa naye mtoto mmoja aitwaye Crespo, hivyo Mafi sango
alitumia jina la mkwewe.
“Safari ya kwenda Maisha Club ilianzia katika Pub moja iliyopo
Kinondoni ambapo tulikuwa watu kama sita au saba kwani walikuwepo Bozy,
Orly, Nyomaa (Gaspar Karemera) na wanawake wawili akiwemo Zai ambaye
alikuwa akituhudumia vinywaji. “Lakini Zai alijiunga nasi katika ile
hali ya kawaida ya kampani na ilikuwa mara yetu ya kwanza kwenda naye
club,” anasema Redondo.
ATUNZA FEDHA NA CHENI YA THAMANI
Wakiwa Maisha Club katika onyesho la Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM
Academia, Mafisango alikuwa akitunza fedha kila mara na waimbaji wakawa
wanamuimba. Bozy ndiye aliyekuwa akitumwa fedha hizo kuzipeleka kwa
waimbaji na ilifi ka wakati kabla hata ya kuwafi kia walikuwa wakianza
kumuimba Mafisango.
Ndipo ulipofi ka muda alitoa cheni yake ya silva ili nayo ipelekwe
kwa muimbaji mmoja, lakini Bozy akahoji vipi aitoe cheni hiyo? Lakini
akaambiwa; “Peleka”. “Alinipa cheni yake ya silva ili nikamtunze
muimbaji mmoja, ilikuwa ya gharama na nilipomuuliza akaniambia nimwambie
muimbaji yule kwamba hiyo ni kumbukumbu yake kwani wanaweza wasionane
tena.
“Tangu mchana alisema anataka kutumia fedha zote alizonazo siku
hiyo hadi ziishe ndipo arejee nyumbani, na kweli hilo alilitekeleza,”
anasema Bozy. Mafi sango alikuwa akigawa dola 100 (sasa ni zaidi ya Sh
220,000) kwa watu mbalimbali aliokutana nao na hata klabu alikuwa akitoa
fedha hizo kwa waimbaji ambao walikuwa rafi ki zake.
REDONDO AONDOKA KLABU
Kabla ya saa 8:15 usiku, Redondo na rafi ki wengine wa Mafi sango
waliondoka Maisha Club kwa kutumia usafi ri mwingine wa kukodi na
kuwaacha wao watano yaani Mafi sango, Orly, Bozy, Nyomaa na yule dada
Zai. Waliendelea na burudani huku wakinywa na kabla ya kuondoka, Orly na
Bozy walikuwa hawaonekani ndipo Mafisango na yule dada wakatoka nje
wakitaka kuondoka.
Baadaye akina Orly waliporudi walipoketi kina Mafi sango na
kutowakuta, waliamua kwenda nje kuwafuata ndipo walipomkuta kiungo huyo
wa zamani wa Simba akiwa amekasirika na kutaka funguo zake za gari huku
akiwataka waondoke.
“Tangu asubuhi mimi ndiye niliyekuwa naendesha gari kwani Mafisango
hakuwa mzoefu wa kuendesha gari Dar es Salaam hasa barabara kuu,
nilisita kumpa funguo ili atuendeshe lakini sikuwa na jinsi. “Aliniambia
yeye ndiye mwenye gari hivyo nimpe funguo, halafu kama kuna kitu kibaya
anataka kimtokee yeye mwenyewe na siyo mtu mwingine pia alisema anataka
aendeshe gari hilo mpaka mwisho wake.
“Hatukuelewa ana maana gani ila tuliona ni jambo la kawaida tu,
nikampa funguo na safari ya kurejea nyumbani ikaanza,” anasema Bozy.
Kabla ya kuelekea Chang’ombe walipitia Kinondoni kwanza kwa Redondo
kumjulia hali kama amefi ka salama halafu wakaendelea na safari yao.
PALE KEKO KUMBE WALIGONGWA
Tofauti na ilivyoripotiwa awali kwamba Mafi sango alikuwa akiikwepa
baiskeli ya matairi matatu maarufu kama Guta, ukweli ni kwamba
waligongwa na gari lingine kwa nyuma.
Kama ilivyoelezwa awali kwamba, Mafi sango hakuwa na uzoefu sana
barabarani hivyo baada ya kugongwa licha ya kuzidiwa na gari, asingeweza
kuchukua hatua yoyote ile zaidi ya kuacha gari liende linavyotaka.
“Ukweli kabla ya ajali ile kuna gari lilitugonga nyuma na dereva wa gari
letu ambaye ni Mafi sango alipoteza uelekeo. “Baada ya kugongwa, Mafi
sango alipoteza uelekeo na gari likaenda kugonga mti lakini kilikuwa ni
kishindo kikubwa mno, gari lililotugonga halikuwa kubwa kama yale y a
mizigo bali lilikuwa gari la saizi ya kati kama Nissan Patrol lakini
lenye ngao kwa mbele.
“Baada ya kile kishindo mimi nilipoteza fahamu kwa muda kama wa
dakika mbili hivi na nilipozinduka nikajikuta nipo nje ya gari chini ya
mchanga, nikarudi katika gari na kumkuta Mafi sango ameumia akiwa
ameinamia usukani,” anasema mmoja wa abiria waliokuwemo ndani ya gari
hilo. Bozy aliyekuwa kwenye gari hilo wakati wa ajali, naye
alithibitisha maneno ya abiria mwenzake kwa kusema: “Ni kweli tuligongwa
kwa nyuma na gari lililotugonga lilikimbia.
“Ninachokumbuka ni kwamba Mafisango alikuwa akiendesha kwa mwendo
wa spidi kati ya 80 hadi 100 na hakuwa mzuri sana barabarani, lakini
licha ya kutokuwa na uzoefu na barabara za Dar es Salaam, huku mwanzo
hakuweza kusababisha ajali hadi tulipofi ka Keko na kugongwa. “Lakini
inauma sana kwani sielewi Mafi sango alikufaje kwani wote hatukuwa
tumefunga mikanda ya usalama,” anasema Bozy.
Abiria wote yaani Zai, Nyomaa, Orly na Bozy hawakuumia sana na wala
hawakutibiwa kwa muda mrefu, lakini Mafi sango alionekana kuumia sana
kichwani katika paji na jichoni. Ikumbukwe kuwa Bozy si aliyetoa maelezo
Polisi bali ni Orly na Nyomaa ndio waliofanya hivyo.
Hakika hizo ndizo saa 24 za mwisho za Mafisango!
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment