Mbwana Samatta ameifungia KRC Genk bao pekee wakati ikiitwanga Eupen katika Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Genk imeshinda 1-0 baada ya Samatta kufunga bao hilo katika dakika ya 82 akiunganisha basi safi ya Ruslan Malinovysky.
Samatta ambaye amecheza kwa dakika zote 90, alionyesha uwezo mkubwa ikiwa ni pamoja na kuwapa wakati mgumu mabeki wa Eupen.
Kama si juhudi za kipa wa Eupen Hendrik van Crombrugge, Samatta ambaye ni nahodha wa Taifa Stars angeweza kufunga mabao mengine.
Kwa
ushindi huo Genk imesogea hadi katika nafasi ya nane ikiwa na pointi
31, huku Club Brugge ikiendelea kuwa kinara wa Ligi Kuu Ubelgiji ikiwa
na pointi 43.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment