Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John
Pombe Magufuli, amesema kuwa serikali imepanga kuondoa msongamano wa
magari Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni pamoja mpango wa kuanzisha safari
ya treni ya mafuta na umeme kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.
Rais Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo leo
Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa awamu ya kwanza ya mradi wa
miundombinu ya utoaji huduma kwa mradi huo wa BRT uliogharimu shilingi
bilioni 403 ambapo amesema ujenzi huo utakuwa ni wa jumla ya kilometa
200 ambapo mchakato wa kumpata mkandarasi umeanza na kuwa awamu ya pili
itakuwa ni njia ya treni inayoelekea katika mkoa wa Dodoma.
Hata hivyo Rais amewataka mawaziri wa ujenzi, Tamisemi na pamoja na uongozi wa DART kuwasilisha taarifa ya faida ya mradi huo kuanza ili kufahamu kama mradi huo unaendeshwa kwa faida au hasara.
"Mawaziri mmetoa taarifa nzuri sana hapa
lakini mmeninyima raha kwa kutonipa taarifa ya pesa za faida
zilizopatikana kutokana na mradi huu" alisema Rais Magufuli
Amesema alitaka kujua kama zipo fedha za faida za mradi huo ili atoe maagizo kuhusu eneo la Kimara kujengwa kituo kingine kikubwa sehemu ya kuegesha magari ili wenye magari binafsi waegeshe na kupata magari ya mwendo wa haraka.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment