Kondakta wa daladala linalofanya safari zake kati ya Nguvumali hadi Raskozone, Salim Kassim amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa ndani ya kambi ya jeshi jijini Tanga.
Kwa
mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, kondakta huyo alikufa wakati
akipelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo na chanzo cha kifo bado
kinachunguzwa.
Imeelezwa
kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku, ambapo mashuhuda walidai kuona
kondakta huyo akichukuliwa na wanajeshi na kuingizwa kambini na baadaye
alitolewa akiwa hajitambui
Akizungumzia
tukio hilo, Khalid Juma mkazi wa Nguvumali jijini hapa alisema askari
hao wamekuwa na desturi ya kuwapiga wananchi bila kuchukuliwa hatua
zozote za kisheria.
“Tumekuwa
tukipata vipigo kila wakati, licha ya viongozi kupata taarifa za
matukio hayo wamekaa kimya na hili tukio ni la tatu kutokea hapa,” alidai Khalid.
Diwani
wa Kata ya Nguvumali ambaye pia ni Meya wa Jiji la Tanga, Alhaji
Mustapha Selebosi alisema sababu za kipigo hicho ni mwanafunzi wa shule
moja jijini Tanga ambaye ni mtoto wa ofisa wa JWTZ kuzozana na kondakta.
==>Zaidi, Tazama Video Hii
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment