Marcus Rashford kinda wa Man United msimu uliopita alionekana lulu.Alikuwa anafunga sana magoli muhimu.Alizifunga timu kubwa kama Chelsea na Manchester United lakini wakati huo Van Gaal pia hakuwa anampa dakika 90 uwanjani.
Hata kocha wa sasa Jose Mourinho naye hampi mda mwingi kucheza uwanjani.Sii kwamba hawamuamini au hawataki ushindi bali kwa kuwa bado kinda wanampa muda mrefu kupumzika.Muda ambao hupungua kadri siku zinavyoenda na baada ya muda atapewa dakika 90.
Shiza Kichuya ni kati ya wachezaji wadogo ambao nilikuwa nawaamini sana na bado namuaminia sana toka akiwa Mtibwa Sugar.Huwa ni mzuri sana akicheza kutokea kishoto,amebarikiwa vitu vingi uwezo wa kukimbia lakini pia anajua kutembea mpira na kutoa pasi sahihi na kwa wakati sahihi.
Usajili wake kwenda Simba haukuwa na mbwembwe nyingi.Hii ilitokana labda na timu aliyotokea au kwa kuwa pia yeye sio mchezaji kutoka nje.Lakini mimi niliuona ni usajili bora kabisa wa Simba msimu huu.Simba ilihitaji mtu ambae atakuwa anaipandisha timu kwa speed(kiberenge).
Aina hij ya uchezaji ni muhimu sana kwani timu ikikosa Plan A kupitisha mipira kati wachezaji wa namna hii hutumika kupigiwa mipira mirefu na kukimbia nayo golini pia wakati wa Counter Attack.Toka aondoke Emmanuel Okwi Simba walikosa mtu wa namna yake ila niliamini Kichuya baada ya mda atakuwa mfalme mpya Simba.
Katika raundi ya kwanza ya msimu wa ligi Kichuya alifunga magoli tisa,magoli hayo ya Kichuya yalifanikiwa kuiweka Simba kileleni mwa ligi na yeye akiwa mfungaji bora raundi iliyopita.
Bao lake la kona dhidi ya watani wao Yanga lilimfanya kichuya aanze kuongelewa karibia kila kona ya jiji.Niliamini Kichuya atauwasha moto Msimbazi lakini sio kwa haraka hivyo.
Baada ya goli dhidi ya Yanga mashabiki waliamini Kichuya kaja kuwasha moto.Matumaini juu yake yaliongezeka nakuonekana mwokozi wao kaja kuwapa ubingwa.Mashaka yangu kwake yalianza,katika ligi ya nchi kama yetu ligi bayo ndani ya wiki mbili waweza cheza mechi nne.
Ligi bayo mapumziko hayaeleweki ni lininikawa siamini kama Kichuya angeweza kuendeleza moto huo.Ila nafsi ikasema nimpe muda.Katika mashindano ya Mapinduzi wasiwasi wangu juu yake ulizidi hakuwa katika kiwango chake mashindano yote.
Mara ya mwisho namuona Kichuya akifunga goli ilikuwa mwezi wa 11 dhidi ya Stand United.Pengine labda hatupaswi kumlaumu kwa kuwa anacheza pembeni.Lakini hata mchango wake katika timu umepungua mno na imenza kutia mashaka kwa Simba katika mbio hizi za ubingwa.
Wakati Kichuya akifunga magoli tisa raundi iliyopita aliwafanya Simba kuonekana tishio sana na aliipeleka kileleni ikitofautiana pointi 8 na Yanga.
Kadri kiwango chake kinavyopungua ndivyo pengo la pointi na watani wao linavyopungua,zimebaki mbili.Kwa Simba hii ambayo wachezaji wa katikati wana utasa wa kutofunga ni ngumu sana kuitabiria Simba Fc ubingwa kwa sasa.Kadri Kichuya anavyopungua makali ndio Msuva anavyoongezeka.
Kichuya sasa hafungi na hata zile nafasi alizokuwa akiwatengenezea Simba hazipo.Ameshachoka,ndani ya muda mfupi sana aliotumika Simba anaonekana kuchoka.Miezi kadhaa iliyopita wakati yuko katika kiwango chake cha juu ilikuwa ukiniuliza kuhusu Simba Fc kuchukua ubingwa bila kupepesamacho ningekuambia Yes lakinj sasa ukija na swali hilo nitaguna tu na kukujibu “Time Will Tell”.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment