Aliyekuwa
Rais wa Gambia, Yahya Jammeh ameondoka nchini humo baada ya mvutano wa
muda kufuatia kushindwa katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika
Disemba Mosi mwaka jana.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na ECOWAS, kiongozi huyo aliyeiongoza
Gambia kwa miaka 22 alipanda ndege kuelekea nchini Guinea ambapo akifika
atasafiri kwenda nchini Equatorial Guinea atakapoishi uhamishoni.
Yahya Jammeh is to go into exile in Equatorial Guinea
Jammeh
alishindwa na kiongozi wa upinzani, Adama Barrow ambaye amekuwa akiishi
nchini Senegal na kueleza kuwa atarudi Gambia usalama ukiimarika.
Barrow
aliyeapishwa katika Ubalozi wa Gambia nchini Senegal, alisema kuwa
akiingia madarakani ataunda tume kuchunguza ukiukwaji wa haki za
binadamu uliofanywa na Yahya Jammeh katika kipindi cha miaka 22 ya
utawala wake.
Rais
wa ECOWAS, Marcel de Souza pia ameeleza kuwa wanajeshi waliokuwa
wametumwa kutoka nchi wanachama kwenda kumuondoa Jammeh madarakani sasa
wataondolewa japo wachache watabaki kuendelea kuimarisha usalama.
Wananchi
wa Gambia wamekuwa na hisia tofauti kuhusu kuondoka kwa Jammeh ambapo
wanaoaminika kuwa ni wafuasi wake walisikitika kwa majonzi alipokuwa
akiwaaga katika uwanja wa ndege huku wengine wakishangilia kuamini kuwa
ni mwisho wa utawala wa kidikteta uliokuwa hauheshimu haki za binadamu.
Kitu
alichoahidiwa Jammeh kuweza kuachia madaraka baada ya kukutana na
baadhi ya viongozi wa mataifa mengine bado hakijafahamika.
Yahya Jammeh anakuwa Rais wa kwanza wa Gambia kuondoka madarakani kwa amani tangu walipopata uhuru mwaka 1965.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment