Kila
kitu sasa safi kwa mshambuliaji Thomas Ulimwengu katika kikosi cha AFC
Eskilstuna kinachoshiriki Ligi Kuu ya Sweden, kwani licha ya kuanza
mazoezi, timu hiyo imemuombea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC)
mchezaji huyo.
Tayari Ulimwengu na kikosi chake cha AFC wako nchini Hispania katika jiji la Barcelona ambako wameweka kambi.
Siku
chache tu baada ya kuanza mazoezi na timu hiyo, timu hiyo imetuma barua
kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiomba ITC ya Ulimwengu ili
aweze kujiunga nao, hii inamaanisha klabu hiyo imekoshwa na uwezo wa
straika huyo.
Ulimwengu
ambaye alikuwa akiichezea TP Mazembe ya DR Congo, alijiunga na timu
hiyo Jumatatu ya wiki hii na kuanza mazoezi juzi Jumatano kwa mujibu wa
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas.
Ofisa
Habari wa TFF, Alfred amesema AFC Eskilstuna imetuma maombi ya ITC ya
Ulimwengu jana na leo hii wanatarajia kuituma ili akaanze kazi yake ya
kucheza soka mara moja.
“Leo
hii (jana) tumepokea maombi ya ITC ya Ulimwengu kutoka AFC Eskilstuna
na hivi sasa tupo katika harakati za kuiandaa hivyo mpaka kufikia kesho
(leo) itakuwa tayari tumeituma,” alisema Alfred.
Ulimwengu amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment