Mkutano wa Sita wa Bunge unaanza Jumanne Januari 31, 2017 na kumalizika
Februari 10, 2017 Mjini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano
huo utaanza na kauli ya serikali kuhusu hali ya chakula pamoja na deni
la taifa na hali ya uchumi nchini.
Mkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kupokea Taarifa za mwaka za
Kamati za Kudumu za Bunge ambapo Kamati 14 za kisekta na mtambuka
zitawasilisha taarifa zake Bungeni katika kipindi hiki.
Shughuli nyingine zitakazofanyika katika Mkutano huu ni kama ifuatavyo:-
KIAPO CHA UAMINIFU
Kufuatia uteuzi wa wabunge watatu walioteuliwa na Mhe. Rais Dk. John
Pombe Magufuli hivi karibuni na Uchaguzi Mdogo uliofanyika katika Jimbo
la Dimani, Zanzibar Tarehe 22 Januari 2017, kutakuwa na Kiapo cha
Uaminifu kwa Wabunge wapya wanne ambao ni:-
Mhe. Alhaji Abdallah Majula Bulembo
Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi
Mhe. Anne Kilango Malecela
Mhe. Ali Juma Ali - (Jimbo la Dimani)
MASWALI
Katika Mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa
na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za
Kudumu za Bunge wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa
Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za Alhamisi.
KAULI ZA MAWAZIRI
Aidha, katika Mkutano huu wa Bunge Kauli mbili za Mawaziri zitawasilishwa kama ifuatavyo:-
Kauli ya Serikali Kuhusu Hali ya Chakula Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.
Kauli ya Serikali kuhusu Deni la Taifa na Hali ya Uchumi Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.
MISWADA YA SHERIA
Katika mkutano huu, miswada ifuatayo itajadiliwa...
Muswada wa Sheria ya Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya
Shirikishi wa mwaka, 2016 (The Medical, Dential and Allied Health
Professionals Bill 2016).
Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na.4) wa mwaka
2016. {The Written Laws (Miscellaneous Amendments)}, Bill, 2016)
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment