Uongozi
wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetoa taarifa kuwa kuanzia saa 9
alasiri leo Januari 30, 2017 njia ya reli kati ya Kituo Kikuu cha Dar es
salaam na Ruvu imefunguliwa rasmi kwa shughuli za uendeshaji wa reli.
Taarifa
hiyo imesema kuwa kazi ya ufunguaji njia imewezekana baada ya Wahandisi
na Mafundi wa reli kuyaondoa Mabehewa yaliopata ajali kutoka relini na
pia kuikarabati sehemu iliyoharibika . Kazi hiyo imefanyika kuanzia
usiku wa Januari 29, 2017 hadi mchana wa Januari 30, 2017.
Aidha
treni ya abiria iliyoahirisha safari ya kuondoka kwenda bara jana
imeondoka leo saa 9:05 alasiri kutoka kituo kikuu cha Dar es Salaam
kwenda bara..
Wakati
huo huo imefahamika kuwa msafiri mmoja aliyetambulikana kama Nd
Basekena O. Bango kutoka Bujumbura Burundi akiwa anasafiri kutoka Kigoma
amelazwa katika Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani wa Pwani kwa ajili ya
matibabu zaidi. Aligunduliwa kuwa amechanika mguu wake wa kulia hivyo
basi kuhitaji kushonwa mguu wake huo.
Taarifa
kutoka Muhimbili zinaeleza kulazwa kwa majeruhi wawili waliopokelewa
hospitalini hapo usiku wa Januari 29, 2017. Majeruhi wamefahamika kuwa
ni Nd. Stephania Mbona (46) kutoka Kigoma alikuwa amekuja Muhimbili
kuendelea na matibabu ya ugonjwa wa tumbo, hata hivyo alitibiwa majeraha
ya kawaida na anaendelea kulazwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wake
wa tumbo.
Mgonjwa
wa pili Nd Alice Jovin (37) mkazi wa Salasala Dar es Salaam alikuwa
anatoka Kigoma kuja Dar es Salaam amepata majeraha ya kawadia ametibiwa
na alitarajiwa kuruhusiwa leo asubuhi.
Kuhusu
idadi ya wasafiri treni ya Deluxe yenye uwezo wa kusafirisha abiria
zaidi ya 1000 wakati inapata ajali ilikuwa na abiria 480.
Aidha
imefahamika kuwa ili kufahamika hasara na sababu za ajali hiyo taarifa
rasmi itatolewa baada ya uchunguzi wa Kamati maalum inayoundwa kwa
mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za uendeshaji reli za kimataifa.
Taarifa hiyo itatolewa baada ya wiki mbili.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Januari 30, 2017
DAR ES SALAAM
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment