Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Serikali
ya Tanzania na Serikali ya Uturuki zimesaini mikataba tisa ya
makubaliano ya kiuchumi inayolenga katika kuimarisha uhusiano na
ushirikiano wa maendeleo baina ya nchi hizo.
Mikataba hiyo inahusisha sekta za uchukuzi, mawasiliano, habari, elimu, utalii, utafiti, viwanda, afya na ulinzi.
Akizungumza
mara baada ya kusaini kwa mikataba hiyo leo Ikulu Jijini Dar es
Salaam, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli
alisema ujio wa Rais wa Uturuki na ujumbe wake ni kielelezo cha ukuaji
wa mahusiano baina ya Tanzania na Uturuki katika nyanja ya biashara na
kimaendeleo baina nchini hizo.
Rais
Magufuli alisema katika mazungumzo yake aliyofanya na Rais Recep
Erdogan kuhusu ujenzi wa Reli ya Standard Gauge nchini, alimjulisha
kiongozi huyo kuwa miongoni mwa wakandarasi walioomba zabuni ya ujenzi
wa reli hiyo kuwa ni kampuni kutoka Uturuki, hivyo endapo itashinda
zabuni hiyo itasaidia kukuza uhusiano uliopo baina ya nchi hizi mbili.
Aidha,
Rais Magufuli alisema kuwa, Serikali ya Tanzania inatarajia kuomba
mkopo kupitia Benki ya Exim ya Uturuki katika kujenga sehemu ya kipande
cha ujenzi wa reli hiyo.
Rais
magufuli alisema Tanzania inaendelea kunufaika na uwepo wa Shirika la
Ndege la Uturuki kwa kufanya safari zake za moja wka moja kutoka nchini
Uturuki, kwa kuwa utasaidia kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini na
hivyo kukuza uchumi wa nchi hizo.
Kwa
upande wake Rais wa Uturuki, Recep Erdogan alisema kuwa uwepo wa
mikataba hiyo baina ya Tanzania na Uturuki itasaidia kupata matokeo
mazuri ya uhusiano pamoja na fursa mbalimbali za ushirikiano katika
nyanja ya Kilimo, Utalii, Ulinzi, Reli ambazo zitawezesha kukuza uchumi
wa mataifa hayo.
Rais
Erdogan alisema kuwa Uturuki imelenga kukuza ushirikiano uliopo baina
yake na Tanzania kupitia makongamano ya wafanyabiashara yenye malengo
ya kukuza uchumi, kuongeza ajira pamoja na kukuza ujasiriamali baina ya
Tanzania na Uturuki.
“Kiwango
cha Biashara ya uwekezaji katika nchi ya Uturuki ni Dola za kimarekani
150 ambapo lengo letu ni kufika Dola za kimarekani 500,” alisema Rais
huyo.
Aidha
Rais Erdogan alisisitiza kuwa kufanya kazi kwa pamoja kutasaidia nchi
hizi kusonga mbele na kufanikiwa katika nyanja mbalimbali.
Nae
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe alisema kuwa
makubaliano ya mkataba baina ya Tanzania na Uturuki katika Sekta ya
Utalii yatasaidia katika kutangaza vivutio vilivyopo nchini,
kubadilishana wataalamu, kubadilishana taarifa na kuongeza idadi ya
watalii nchini.
Prof.
Magembe aliongeza kuwa makubaliano hayo yatakuza sekta ya utalii katika
kuvutia uwekezaji wa katika maeneo ya hoteli, fukwe na mbuga za wanyama
zilizopo nchini.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment