Desemba 6, mwaka jana Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
alipata mtoto wa pili kupitia kwa mzazi mwenzake, Zarina Hassan ‘Zari’
na kumpa jina la Nillan Nasibu ‘Chibu Junior’, akiwa ametanguliwa na
dada yake, Latifah ‘Tiffah’ aliyezaliwa Agosti 6, 2015.
Kwa hesabu za harakaharaka, Januari 16, mwaka huu, Nillan alikuwa
anatimiza siku 40 tangu kuzaliwa kwake, lakini siku hiyo imepita
kavukavu huku wadau wake waliokaa mkao wa sherehe wakibaki na maswali
bila majibu.
SHUGHULI ILIKUWA KWENYE RATIBA
Wiki chache zilizopita, iliripotiwa kwamba, Diamond kwa maana ya
baba wa mtoto, aliandaa sherehe ya kufa mtu ambayo ingefanyika jijini
Johannesburg, Afrika Kusini ‘Sauzi’ ambako mtoto huyo alizaliwa.
“Lakini kinachotushangaza wadau ni kwamba, mpaka siku zinakaribia hakuna dalili na matokeo yake, siku imepita hakuna lolote.
“Tulipewa kadi watu ambao tungekwenda Afrika Kusini kwenye
shughuli. Lakini naona kimya kingi mpaka Januari 16 imepita. Hakuna cha
40. Hata kama shughuli itafanyika Jumamosi hii (keshokutwa) itakuwa si
40 tena, bali ni 45 sasa,” kilisema chanzo hicho.
TOFAUTI NA TIFFAH
Baadhi ya wadau wa staa huyo sambamba na mashoga zake Zari waliliambia Amani kuwa, ujio wa Nillan hauna ‘vurugu’ kama ilivyokuwa kuzaliwa kwa Tiffah ambaye nchi ilisimama.
Siku ya 40 ya Tiffa
“Unajua huenda 4O ikawa imepoteza mvuto baada ya ile ya Tiffah
kuchukua nyota yote. Utakuwa unakumbuka mwandishi kwamba, kuzaliwa kwa
Tiffah Bongo ilitulia kimya. Hata siku ya 40 yake kule nyumbani na
baadaye kwenye ile shughuli ya Mlimani City, jina la Tiffah lilikuwa juu
sana.”
Siku ya 40 ya Tiffa
WENGI HAWAMJUI NILLAN
“Lakini sasa we fanya utafiti wa kawaida tu, Wabongo wengi
hawalijui jina la Nillan ambaye ni mdogo wake Tiffah. Hakuna mbwembwe
wala matangazo,” kilisema chanzo.
Prince Nillan Dangote
MABENKI YAMECHANGIA?
Habari zaidi zinasema kuwa, mbwembwe za Tiffah mwaka juzi
zilichangiwa na mabenki yaliyojitoa kumwaga pesa kwa ajili ya kuchukua
haki ya kwanza ya kumwonesha sura mtoto huyo ambapo tofauti na ujio wa
Nillan, hali ya mabenki imekuwa mbaya kiasi kwamba, yale mawili
yaliyotaka kuchukua haki hiyo yaliingia mitini.
“Ukifuatilia kwa karibu hapo utabaini kuwa, kutojitokeza kwa
mabenki hayo kumwaga pesa pia kumechangia kudorora kwa vuguvugu la
kuzaliwa kwa mtoto Nillan.
“Unajua hali ya uchumi ni mbaya kwa sasa, nadhani hata Diamond
mwenyewe anajiuliza kama akifanya sherehe kubwa ya 40 halafu akatumia
mfano milioni hamsini kama staa yeye atafaidika na nini? Sherehe tu?
Maana kama ni mtoto anaye tena ni wa pili huyu.”
MAMA DIAMOND AREJEA BONGO, AJICHIMBIA MADALE
Awali ilidaiwa kuwa, baada ya mama Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’
kwenda Sauzi kusubiria Zari kujifungua Nillan, ratiba ilimtaka aendelee
kutulia kulekule akisubiri 40 ambayo ingefanyika kule lakini habari
zinadai kutokana na kutokuwepo kwa ishu hiyo, mwanamke huyo amerejea
kimyakimya Bongo na amejichimbia Madale nyumbani kwa mwanaye.
Diamond, mama Daimond kulia Rommie Jons
“Kama mnataka kujua kuwa 40 imebuma, hata mama Diamond amerudi.
Hivi ninavyoongea na wewe mwandishi, mama amejaa tele Madale. Hakuna
mbwembwe. Ama kweli hali ya uchumi wa mifuko ni mbaya jamani,” kilisema
chanzo.
ZARI NAYE ATUA BONGO
Habari zaidi za chini kwa chini zinasema kuwa, mama Nillan, yaani
Zari naye ametua Bongo bila mbwembwe hali inayotoa taswira ya kutokuwepo
kwa shughuli achilia mbali sherehe.
BABA DIAMOND AFUNGUA BEGI
Ikazidi kudaiwa kuwa, baada ya kuvunjika kwa safari ya Sauzi, baba
wa Diamond, mzee Abdul ambaye aliwahi kuripotiwa kuwa, amekaa mkao wa
safari, ilibidi afungue begi na kutoa viwalo vyake kisha kuendelea na
maisha yake ya kila siku, Bongo.
MADAI YACHUNGUZWA
Ilibidi Amani lishike nyuzi hewani ili kuwasaka
wahusika hao. Mtu mgumu sana kupatikana katika wote ni Zari ambaye
uchunguzi unaonesha kuwa, hata wale madansa wa Diamond, akina Moses
Iyobo hawana namba yake au wamepigwa marufuku kwa kiapo kuigawa.
Hivyo Amani lilimtafuta Diamond mwenyewe kwa njia ya simu yake ya mkononi iliyoita weee mpaka ikakatika bila kupokelewa.
Amani likaona isiwe shida, likamtumia meseji (SMS)
kwa kuamini kwamba, kama alipopigiwa alikuwa anaoga, anaendesha gari,
anapafomu au yuko faragha, baada..
ya kuiona meseji hiyo angejibu lakini wapi!
MAMA DIAMOND
Ndipo Amani likamgeukia mama Diamond mwenyewe
ambaye ndiye anayetajwa kusimamia maandalizi ya shughuli au kuamua
kutosimamia kuandaa ambapo hali ilikuwa hivi:
Amani: (latoa utambulisho wa jina na chombo cha habari).
Mama Diamond: Aha! Niambie, unataka kunifundisha uandishi wa habari?
Amani: Ndiyo.
Mama Diamond: Haya nipe habari, nakusikiliza.
Amani: Napenda kujua, kuna madai kwamba, shughuli
ya 40 ya mdogo wake, Tiffah imeota mbawa, hakuna. Je ni kweli au
imeshafanyika kimyakimya?
Mama Diamond: (akakata simu).
Amani liliamini kuwa, huenda simu hiyo imekatika
kutokana na hali ya mtandao, likaacha zikatika dakika kumi kwanza kabla
ya kupiga tena.
Baada ya dakika kumi kupita…
Mama Diamond: We nani?
Amani: Mimi ni …(utambulisho wa jina na chombo cha habari).
Mama Diamond: (akakata simu).
BABA DIAMOND
Kwa upande wake, baba Diamond alipotafutwa na kuulizwa kuhusu
safari hiyo alisema yeye ni msikilizaji kama safari ipo angekwenda kama
haipo pia hana neno.
“Mimi ndugu yangu ni wa kusikiliza tu. Kama safari ipo nakwenda,
kama haipo hakuna neno. Kikubwa ni kumwomba Mungu atupe uzima,” alisema.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment