Wakati
imeelezwa kuwa waokoaji katika mgodi wa dhahabu wa RZ Union ulioko
Geita , wamebakiza mita tatu kuwafikia waliofukiwa Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Medard Kalemani akizungumza na ndugu wa watu
waliofukiwa amesema kwamba wanafanya mpango wa kuwapelekea chakula
wachimbaji hao.
Amesema
kwamba jana wamefanikiwa kufanya mawasiliano na wachimbaji hao na
kwamba wapo kumi na watano na kuwa wanachohitaji kwa sasa ni chakula.
Alisema
waokoaji walifanikiwa kuwafikishia kamba na kalamu watu hao ambao
waliandika majina na mahitaji yao na kusema kwamba wote wapo salama.
Watu
hao akiwemo raia wa China mmoja walifukiwa na kifusi juzi usiku baada
ya udongo kukatika na kuziba mlango waliokuwa wakitumia kuingia na
kutoka na uokoaji unaendelea kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya
uokoaji.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment