Rais
wa Guinea, Alpha Conde amechaguliwa leo kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja
wa Afrika (AU), uchaguzi uliofanyika katika vikao vya viongozi wa nchi
wanachama vinavyoendelea katika Makao Makuu ya umoja huo mjini Addis
Ababa nchini Ethiopia.
Rais Conde anapokea uongozi kwa Rais wa Chad Idris Deby ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa umoja wa hadi.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Afrika ni kiongozi asiye na maamuzi (ceremonial head of the
Union). Mwenyekiti huyu huchaguliwa na Marais wa Nchi wanachama wa AU
ambaye hushika wadhifa huo kwa mwaka mmoja tu. Uongozi huu huenda wa
zamu katika Kanda tano za bara la Afrika (Kaskazini, Kusini, Mashariki,
Magharibi, na Afrika ya Kati).
Nafasi hii ilianzishwa mwaka 2002 ambayo Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki ndiye alikuwa mwenyekiti wa kwanza.
Rais
wa Chad, Idriss Deby (kushoto) akikabidhi madaraka kwa Mwenyekiti mpya
wa Umoja wa Afrika, Rais Alpha Conde wa Guinea (kulia).Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment