KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog ameshusha presha ya mashabiki wa timu
hiyo kwa kuwataka kuwa watulivu kwa kuwa bado wana nafasi ya kurekebisha
makosa yao na kutimiza lengo ambalo ni ubingwa.
Simba inashika nafasi ya pili nyuma ya mahasimu wao Yanga, baada ya
Jumamosi kufungwa bao 1-0, na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu, ya
Tanzania Bara, uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Yanga imekamata usukani baada ya kuifunga Mwadui ya Shinyanga juzi kwa
mabao 2-0 na kufikisha pointi 46 na kuiondoa Simba kileleni ambayo ina
pointi 45 baada ya kipigo cha Jumamosi.
Akizungumza Omog, ambaye amekuwa katika wakati mgumu kufuatia kipigo
hicho alisema hata yeye pamoja na wachezaji wameumizwa na matokeo hayo,
lakini mpira ni mchezo wa makosa na kilichobaki kwa sasa ni kujipanga
upya ili kuhakikisha wanafikia malengo waliyokusudia mwishoni mwa msimu
huu.
“Hakuna anayependa kufungwa au kutolewa kwenye nafasi nzuri , lakini
mashabiki wanapaswa kujua Simba siyo lazima kila siku ishinde ingawa
malengo yetu ni ushindi, hivyo inapotokea tumepoteza mchezo kama
ilivyotokea Jumamosi tunatakiwa tukubaliane na matokeo alafu tujipange
kwa mechi nyingine,” alisema Omog.
Mcameroon huyo alisema, kipindi hiki walichokuwa nacho siyo cha
kutupiana lawama bali ni muda wa kuongeza mshikamano na kuisapoti timu
yao kwa kuja kwa wingi uwanjani ili kuweza kushinda mechi zao na kuitoa
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment