Muigizaji na mchekeshaji maarufu nchini Steve Nyerere amemuombea
msamaha msanii wa muziki Nay wa Mitego kwa kuwaita wasanii wa filamu
wote walioandamana kupinga uingizwaji wa filamu kutoka nje ya nchi kuwa
ni 'Matahira'
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Steve Nyerere
amesema kwamba yawezekana Nay wa Mitego alikuwa na hasira hivyo
akashindwa kutumia lugha sahihi ya kuwaelekeza wasanii wenzake
walivyokuwa wanakosea ndio maana alitoa lugha yenye maneno makali
ijapokuwa alikuwa sahihi kukosoa maandamano yale.
"Kwanza naomba nimuombee msamaha ndugu yangu Nay wa Mitego, hakuwa na
nia mbaya lakini hakutumia maadili kufikisha ujumbe wake, Unajua sisi
watanzania hatupendi kuambiwa ukweli na hata tukisemana tuna lugha zetu
laini za kusemeshana. Nay wa Mitego mpaka kutoa maneno makali vile ujue
anaipenda tasnia yetu ya filamu alikuwa kaaumia, si unajua hata yeye
alishawahi kuwa huku anatuonea huruma na anatupenda mimi niseme
mumsamehe tuu" - alisema Steve.
Aidha Steve Nyerere ameongeza kuwa kwa hali ilivyo katika tasnia ya
filamu Tanzania hakuna haja ya maandamano pamoja na kurushiana maneno
kwenye mitandao bali kinachotakiwa ni kukalishana chini waigizaji wote
na kuangalia mahali walipojikwaa na kufanya marekebisho.
"Mtandaoni hatutaweza kumaliza hili tatizo kinachotakiwa hapa ni tukae
chini na tuongee tunataka nini. Msibague kuandamana kwa ajili ya faida
yenu wenyewe ila tujenge hoja ambayo tukubaliane wote tuiombe serikali
itusaidie wote kwa ujumla na siyo watu wachache wanaojifanya manabii
hawataki kukosolewa" Steve Nyerere alisistiza.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment