Korea Kusini imesema wanajeshi wa Marekani wameanza kujenga mtambo wa
kisasa wa kuzuia makombora katika eneo moja kusini mwa nchi hiyo.
Mtambo huo wa kujilinda dhidi ya makombora ambao hufahamika kitaalamu
kama Terminal High Altitude Area Defense (THAAD) unasimikwa kutokana na
wasiwasi wa tishio kutoka Korea Kaskazini ambayo imeendelea kufanyia
majaribio makombora yake.
Wizara ya Ulinzi ya Korea Kusini imesema mtambo huo utakamilishwa na kuwa tayari kutumika katika kipindi cha mwaka mmoja.
Mtambo huo unajengwa katika Wilaya ya Seongju lakini China imekuwa ikipinga kuwekwa kwa mtambo huo.
Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba Marekani iko tayari
kuchukua hatua kivyake bila kuishirikisha China kukabiliana na tishio la
nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment