Friday, 28 April 2017

Fahamu: Kisiwa kilichotumika kuwaadhibu wasichana Uganda.

Wasichana waliokuwa wakishika mimba kabla ya kuolewa walikua wakisadikika kuleta aibu katika familia kwenye baadhi ya maeneo nchini Uganda.

Kutokana na hali hiyo ya kuiletea familia fedheha, wasichana walikuwa wakichukuliwa na kupelekwa katika kisiwa kidogo nchini humo na kuachwa hadi kufa.

Katika jamii ya Bakiga, mwanamke anapaswa kushika mimba baada ya kuolewa.Kuoa msichana aliye bikra kulimaanisha kupokea mahari iliolipwa kwa kutumia ng’ombe. Mwanamke ambaye alishika mimba alionekana kutia aibu na kuipokonya mali familia.

Bi Mauda Kyitaragabirwe mwenye umri wa miaka 80, ni mmoja ya wanawake aliyewahi kuwekwa katika kisiwa hicho cha adhabu.
”Wazazi walipogundua kwamba mimi ni mjamzito waliniweka katika mashua na kunipeleka katika kisiwa cha Akampene. Wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 12 nikiishi katika kisiwa hicho kwa siku nne bila chakula wala maji kwa siku nne”, anasimulia Bi Kyitaragabirwe.

”Nakumbuka katika Siku ya tano mvuvi mmoja alikuja na kusema atanichukua na kunipeleka nyumbani. Nilihofu sana, na nilimuuliza iwapo alikuwa ananidanganya na kwamba alitaka kunitupa kwenye maji, lakini alisema hapana nakuchukua ili kukufanya mke wangu” alieza Bibi huyo kwa mtangazaji wa BBC Swahili.
Kutokana na umbali wa eneo hilo tabia hiyo iliendelea hata baada ya wamishenari na wakoloni kuwasili nchini Uganda katika karne ya 19 na kuisitisha.Watu wengi wakati huo hususani wasichana walikufa kwa kutokujua kuogelea ilikujiokoa.

Na Laila Sued.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

0 comments:

Post a Comment