Friday, 28 July 2017

Msukuma nurusa amchape makonde Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji.

MBUNGE wa jimbo la Geita Vijijini na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita,Joseph Kasheku Musukuma nurusa amchape makonde hadharani Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Ihumilo kata ya Nkome Wilayani humo Thomas Halila, muda mfupi baada ya Mbunge huyo kuongoza mamia ya wananchi wa kijiji hicho kungíoa vigingi vilivyowekwa kwenye mipaka ya eneo la Serikali ya kijiji hicho linalodaiwa limeuzwa kinyemela Tsh. Million sita (600,000.),na mwenyekiti Halila, wakishirikiana na mtendaji wa kijiji hicho Charles Mbilingi kwa kutumia Muhtasari wa majina na saini hewa za wakazi wa kijiji hicho.

Hatua ya Mbunge huyo kuongoza,mamia ya wananchi wa kijiji hicho kisha kungíoa vingingi kwenye eneo hilo lenye ukubwa wa hekali moja na nusu ilikuja baada ya malalamiko ya wananchi hao kudai kutoshirikishwa na kwamba majina yaliyomo kwenye muhtasari wa kikao hicho na hata saini ni za kughushi hali iliyomlazimu Mbunge huyo kusoma jina moja baada ya jingine ili kubaini janja nyani iliyofanywa na mwenyekiti pamoja na mtendaji huyo.

Ambapo iligundulika,mhtasari uliotumika kuuza eneo hilo ni wa kughushi kutokana na wananchi hao kukana kushiriki kikao hicho kilichoketi 15/07/2017 kubariki uuzwaji wa eneo hilo mbali na majina yao kusomwa hadharani,huku diwani wa kata hiyo Masumbuko Sembe akigeuka mbogo baada ya jina lake kuwa miongoni mwa yaliyosomwa na Mbunge wao.

Kufuatia udanganyifu huo, Mbunge huyo akalazimika kuongoza wananchi kwenda kungíoa vingingi vilivyowekwa kwenye mipaka ya eneo hilo lililouzwa kwa mtu ambaye hakufahamika kwa majina wala makazi yake,sambamba na kumwagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo Deus Seif kuondoka na mtendaji huyo.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Mke wa Mugabe Amtaka Mumewe Kumtangaza Mrithi.

Rais wa Zimabwe ametakiwa na mkewe kumtaja ''mrithi'' wake ili kupunguza migawanyiko kuhusu mtu atakayemrithi.


''Rais hafai kuwa mwoga kumchagua mrithi wake na neno alke litakuwa la mwisho'',alisema bi Grace Mugabe.


Bwana Mugabe ndio kiongozi mzee zaidi na chama chake cha ZANU PF kimemchagua kuwania urais kwa mara nyengine mwaka ujao.


Lakini makundi pinzani yamekuwa yakiwania urais ili kuimarisha uwezo wao huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hali yake ya kiafya.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

PENZI ni Kikohozi...Nisha Amuonyesha Mpenzi wake Mpya.

MSANII wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amebadili jina lake na kujiita Nisha Minhal Azad huku kisa kikidaiwa kuwa amefanya hivyo baada ya kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na ‘Serengeti Boy’ anayetumia jina hilo.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na msanii huyo, Nisha amekuwa karibu na ‘Serengeti Boy’ huyo ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva na kwamba ameamua kuanika kabisa uhusiano huo bila kificho.

“Nisha amepata tulizo baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuwa na mwanaume. Huyo mpenzi wake wa sasa ni msanii wa Bongo Fleva anajulikana kwa jina la Minu, yaani Nisha humuelezi chochote juu ya dogo huyo na wanaongozana mara kwa mara,” kilidai chanzo na kuongeza;


“Kwa sasa ameamua kuanika ukweli huo kila kona, kwenye mitandao ya kijamii amebadilisha mpaka jina lake na kujiita Nisha Minhal Azad. Hivi karibuni aliweka picha katika Insta yake akiwa naye katika pozi la mahaba na kuandika; ‘kuna tofauti kubwa kati ya Serengeti na Ngorongoro.’

Baada ya kunasa madai hayo, Ijumaa lilimtafuta Nisha na kumuuliza ukweli juu ya kinachoonekana na kuongelewa, alipopatikana alikiri kubadili jina na kuwa katika uhusiano na Serengeti Boy huyo;
“Ni kweli nipo katika uhusiano na huyo mtu, mengine siwezi kuyaanika ila kifupi ni hivyo.”

Nisha kwa nyakati tofauti aliwahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elbariki ‘Nay wa Mitego’ pamoja na Baraka Andrew ‘Barakah The Prince’.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

TUNDU Lissu Afunguka Baada ya Kutoka Rumande.

Tundu Lissu anasema baada ya kukamatwa na jeshi na polisi alizungushwa sana polisi na mwisho wa siku walimpeleka sehemu katika kituo cha afya ili apimwe mkojo lakini anadai alikata kupimwa mkojo kwani alikuwa anatuhumiwa kwa kosa la uchochezi  lisilo husiana na kipimo cha mkojo.

"Nilizungushwa sana siku ile lakini mwisho wa siku nikapelekwa maeneo ya Ocean Road hospitali ya kansa nikaambiwa Mhe. tunahitaji tukupime mkojo wako, nikamwambia nyie askari mimi nimeshtakiwa kwa uchochezi hivyo kupima mkojo unathibitishaje uchochezi kwa kupima mkojo. Wakasema sisi kuna vitu tunavitafuta, nikawaambia kama kuna vitu mnatafuta wakanishtaki kwanza kwa hilo kosa  ili sasa muende kwa hakimu mkamwambie kuwa mnawasiwasi na mimi kuna vitu mnavitafuta mnaweza kuvipata kwenye mkojo wangu, ila kama hajampata 'order' ya hakimu kwangu mkojo hamjapata" alisema Tundu Lissu 

Aidha Mhe Tundu Lissu anasema kuwa walikuwa wanafanya hivyo ili wapate vitu vya kuandikwa kwenye vyombo vya habari kwamba amepimwa mkojo ili waone kama kuna dalili za madawa ya kulevya na kusema ingewezekana Polisi wakasema kuwa yeye anaongea maneno mabaya kwa kuwa anatumia dawa ya kulevya.

Tundu Lissu aliendelea kulituhumu jeshi la Polisi kuwa wapo baadhi ya polisi wanatengeneza sana kesi na kuwabambikia watu kesi na kutengeneza ushahidi wa uongo
Hata hivyo Tundu Lissu amesema kuwa yeye mwenyewe hapendi kulala rumande na kuacha sehemu nzuri ya kulala yeye na familia yake, anadai kuwa hapendi kukamatwa na polisi wala kulala rumande wala magereza lakini kwenye masuala ya msingi yupo tayari kwa lolote lile.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

MWIMBAJI Lulu Diva Adaiwa Kutoka Kimapenzi na Mwimbaji Jaguar wa Kenya.

BAADA ya kuweka hadharani kuwa amepata meneja mpya katika za muziki, msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ anadaiwa kutoka kimapenzi na meneja huyo ambaye pia ni mwanamuziki kutoka Kenya, Jaguar.
Kwa mujibu wa chanzo, hivi sasa mrembo huyo amejiweka kwa Jaguar na hivi karibuni alipewa kipondo na bwana’ke wa zamani baana ya kubaini uhusiano huo.


“Safari zake Kenya zimekuwa haziishi, wenyewe wanadai wapo kikazi lakini mhh si kwa mapozi ya kimahaba wanayoonesha,” kilibonyeza chanzo na kuahidi kuwabofya picha akiwaona tena.
Baada ya kunasa madai hayo, Star Mix lilimtafuta Lulu na alipopatikana alisema;
“Ni uzushi kama unavyojua Wabongo, Jaguar ni meneja wangu tu ambaye ananisaidia katika kunisimamia katika muziki na si vinginevyo.”

Na Imelda Mtema

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

MTEJA Amuua Mganga wa Kienyeji Baada ya Kushindwa Kumtibu.

Mganga wa jadi, Revocatus Kanjalanga (65) katika Wilaya ya Nkasi mkoani Ruvuma ameuawa kikatili kwa kuchomwa na mkuki mgongoni na mtu asiyefahamika ambaye anadaiwa kuwa ni mteja wake wa muda mrefu.

Ilielezwa kuwa wateja wa mganga huyo walikuwa wakimlalamika kuwa kwa kipindi kirefu mganga huyo amekuwa akiwatibu kwa kuwatoza fedha nyingi za malipo ya matibabu lakini wamekuwa hawaponi kupitia uganga wake.

Mtoto wa mganga huyo aliwaambia waandishi kuwa baba yake aliuawa juzi saa 1:30 asubuhi kwa kupigwa mkuki mgongoni akiwa anatembea mitaani katika kitongoji cha Chawe kilichopo katika Mji wa Namanyere wilayani Nkasi.

Alisema kuwa kwa muda mrefu watu ambao walikuwa wanatibiwa na baba yake walikuwa wakilalamika kutozwa fedha nyingi pamoja na mifugo lakini hawaponi, hali iliyosababisha kuanza kumuona kama tapeli.

Alisema watu hao walikuwa wanalalamikia kutofanikiwa matatizo yao ya kiafya, kutafuta mali pamoja na mazindiko.

“Pengine malalamiko hayo ndiyo yaliyosababisha mtuhumiwa aamue kumuua kwa kumchoma mkuki mgongoni, na aliyefanya hilo hajapatikana na mpaka sasa anatafutwa,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anasakwa.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

KISHINDO Kingine Makinikia Chaiva...Vigogo wa Kampuni ya Barrick Gold Watua Nchini.

KISHINDO kingine kuhusiana na sakata la usafirishaji wa mchanga wa madini (makinikia) kwenda ughaibuni kimeiva baada ya kuwapo kwa taarifa za ujio wa vigogo wa kampuni ya Barrick Gold nchini ili kuanza tena mazungumzo mazito na serikali.

Hivi karibuni, Serikali ilitangaza kuzuia usafirishaji makinikia kwenda ughaibuni na pia Mamlaka ya Mapato (TRA) kuwataka Barrick, ambao humiliki hisa nyingi za kampuni ya Acacia Mining, kulipa kodi na adhabu inayofikia jumla ya dola za Marekani bilioni 190, sawa na zaidi ya Sh. trilioni 400.

Kodi hiyo ni matokeo ya taarifa zisizokuwa sahihi kuhusiana na madini yaliyochimbwa kuanzia mwaka 2000 -- kiasi ambacho kilibainishwa na ripoti za kamati mbili teule za Rais kuchunguza makontena 277 ya makinikia yaliyozuiliwa kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Taarifa ambazo Nipashe ilizipata jana na kuthibitishwa na Barrick na Acacia, ni kwamba viongozi wa juu wa Barrick wanatarajiwa kutua nchini wiki ijayo ili kuendelea na mazungumzo na serikali kwa nia ya kufikia mwafaka juu ya suala hilo.

Nipashe inatambua kuwa ikiwa ujio huo wa Barrick utafanyika wiki ijayo, itakuwa ni siku chache baada ya Rais John Magufuli kutangaza wazi akiwa katika ziara zake mkoani Kigoma kuwa anaweza kutaifisha migodi yote ya wawekezaji hao na kuwapa Watanzania ikiwa watachelewa kufanya mazungumzo kwa lengo la kulipa mapato ya serikali yaliyopotea katika kipindi chote tangu waanze shughuli zao nchini.

“Kwa sasa tumewaita wafanye mazungumzo wamekubali, lakini wakichelewa nitafunga migodi yote, ni mara kumi migodi hii tukaigawa kwa Watanzania wachimbe wao wauze tupate kodi kuliko hawa wawekezaji ambao hawalipi kodi,” alisema Rais Magufuli.

Akizungumzia ujio huo wa vigogo wa Barrick nchini, mmoja wa maofisa wa Acacia aliiambia Nipashe jana kuwa hawashiriki moja kwa moja kwenye mazungumzo hayo, lakini chochote kitakachoamriwa watakiridhia.

Aidha, katika ripoti ya mapato ya robo mwaka ya Barrick iliyopo kwenye tovuti yao, imeelezwa kuwa wataendelea na mazungumzo na Serikali ya Tanzania kuanzia wiki ijayo kuhusu makinikia yaliyozuiliwa kusafirishwa nje na mambo mengine yanayohusu utendaji wa kampuni hiyo nchini.

Mbali ya hilo, kampuni hiyo ilielezea mwenendo wa biashara kwa kipindi kilichomalizika Juni 30 mwaka huu kuwa ni mzuri, licha ya kuongezeka kwa gharama za uchimbaji dhahabu kwa asilimia 10.

Makubaliano ya kufanyika kwa mazungumzo kati ya Barrick na Serikali yalitokana na kikao kilichofanyika Juni 14, mwaka huu Ikulu jijini Dar es Salaam, kati ya Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Barrick, Prof. John Thornton.

Katika mazungumzo hayo, Prof. Thornton alisema kampuni yake iko tayari kufanya mazungumzo na Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza.

Mazungumzo hayo yalifanyika zikiwa zimepita siku tatu baada ya Rais Magufuli kukabidhiwa ripoti ya pili ya mchanga wa madini na kamati ya pili aliyoiunda kuchunguza suala hilo.

Alipoulizwa kuhusu ujio wa viongozi wa Barrick, Kamishna wa Madini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka, alijibu kuwa suala hilo haliratibiwi na wao.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, ambaye alisema atafutwe Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani ili azungumzie ujio huo mwingine wa viongozi wa Barrick.

Hata hivyo, jitihada za gazeti hili kumpata Dk. Kalemani zilishindikana jana baada ya kukosekana kupitia simu yake ya mkononi.

Source: Nipashe

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

#BREAKING News>>>Wasira Aangukia Pua Tena...Rufaa Yatupiliwa Mbali.

Mahakama ya Rufani imetupia mbali rufaa iliyokatwa na wapiga kura 4 wa Jimbo la Bunda Mjini kupinga ushindi wa Mbunge, Esther Bulaya.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Thursday, 27 July 2017

BAADA YA KUONA MAMBO SI SAFI, CHELSEA WAREJEA GYM TENA.

Mabingwa wa England, Chelsea imeendelea na mazoezi na sasa wako gym.

Chelsea imerejea gym kwa ajili ya kuongeza nguvu baada ya kucheza mechi kadhaa za michuano ya ICC.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imewateua 8 kuwa Wabunge wa Viti Maalum CUF.

Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na kifungu cha 86(8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 27 Julai 2017imewateua wafuatao kuwa Wabunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF).

1- Ndugu Rukia Ahmed Kassim;
2- Ndugu Shamsia Aziz Mtamba;
3- Ndugu Kiza Hussein Mayeye;
4- Ndugu Zainab Mndolwa Amir;
5- Ndugu Hindu Hamis Mwenda;
6- Ndugu Sonia Juma Magogo;
7- Ndugu Alfredina Apolinary Kahigi; na
8- Ndugu Nuru Awadh Bafadhili,

Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo kwa nafasi waza nane (8) za Wabunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Wananchi CUF.

Jamii Forums

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

SHAMSA Ford Awachana Wanaume Wanaopenda Kulelewa.

Msanii wa Filamu nchini, Shamsa Ford amewatolea uvivu wanaume wanaopenda kulelewa na wanawake.

Kupitia mtandao wa Instagram muigizaji huyo ameonyeshwa kukerwa na tabia hiyo ambayo inapekea wawe tegemezi kwa wapenzi hao kutokana na kuchagua kazi.

“Kaka zangu na wadogo zangu wa kiume ningependa kuwashauli mpende kujituma na kufanya kazi kwa bidii, usitamani kazi ya kuzunguka kwenye kiti ofisini wakati elimu yako ni darasa la pili. Mwanaume unatakiwa ujitume na kupambana na maisha, sukuma hata mkokoteni ilimradi ujipatie riziki.,” ameandika mrembo huyo.

Akaongeza “Sasa nyie kaka zangu wa sasa hivi yaani hampendi kufanya kazi ukishajiona una sura nzuri basi na wewe eti unadanga kwa jimama lenye pesa. Sasa kama mwanamke anakufuga wewe unadhani atakuheshimu?utachezea kuchapwa vibao na kutukanwa, hivi hamuumii na haya majina mnayoitwa?mara vibenten,vipanyabuku,vichura,vitom and jerry…daah.”

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

ACACIA yalipa Milioni 460 za ushuru.

Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu (BGML) uliopo katika Halmashauri ya Msalala, mkoa wa Shinyanga jana Jumatano Julai 26,2017 umekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi 460,732,841.08/= kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo,Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew alisema kiasi hicho ni asilimia 67 ya malipo ya ushuru wa huduma kwa ajili ya kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi mwezi Juni mwaka huu ambacho ni asilimia 0.3 ya ukokotoaji wa ushuru wa huduma wa mgodi huo katika kipindi hicho.
 
 “Jumla ya malipo ya ushuru wa huduma kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ni shilingi za Kitanzania 687,660,956.84/=,ambapo malipo hayo yamegawanywa katika halmashauri mbili ambazo ni Msalala inayopata asilimia 67 na Nyang’wale iliyopo mkoani Geita inapata asilimia 33”,alifafanua Crew.
 
Alisema kutokana na mgawanyo huo,halmashauri ya Msalala imelipwa shilingi milioni 460 (460,732,841.08/= ) na Nyang’wale shilingi Milioni 226 (226,928,115.76/=.
 
“Ushuru umepungua kwa kuwa mgodi haujafanya mauzo ya makinikia ambayo yamezuiwa tangu mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu, hivyo tunafahamu kuwa tutalipa zaidi tutakapouza makinikia ambayo yapo yanaendelea kukusanywa mgodini”,aliongeza Crew.
 
Katika hatua nyingine Crew alisema tangu mwaka 2000 mpaka sasa mgodi huo umelipa zaidi ya shilingi 10,247,742,957/= za kodi ya ushuru wa huduma na kampuni ya Acacia ilianza kutoa malipo ya ushuru wa huduma wa asilimia 0.3 ya mapato ghafi kwa halmashauri husika mwaka 2014.
 
 “Mgodi wetu unaendelea kuwa na matarajio ya kuchangia kuimarisha sekta ya viwanda kwenye uchimbaji madini katika halmashauri ya Msalala huku tukiendelea kutekeleza mkakati wa Jamii Endelevu wa Acacia ulioanzishwa mwaka 2016 kwa kushauriana na wadau lengo likiwa ni kuchangia maendeleo ya Jamii Endelevu inayonufaika na kukua kwa uchumi ndani ya jamii ili kujenga mahusiano ya kuaminika”,alisema Crew.
 
Akipokea hundi hiyo kisha kuikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliushukuru mgodi wa Acacia Bulyanhulu kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kutoa huduma kwa jami.
 
“Hiki kiwango cha shilingi milioni 460 tulichopokea ni kiwango kizuri ingawa kimepungua ulikinganisha na kipindi cha miezi sita cha Mwezi Juni hadi Desemba 2016,furaha inatujaza kwamba ile shilingi milioni 300 na zaidi ipo ndani ya Makinikia, yatakapouzwa tutaipata na tutaendelea kuboresha huduma za kijamii”,alieleza Nkurlu.
 
Nkurulu alimuomba mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala kuhakikisha fedha zilizotolewa na mgodi huo zitumike kwa huduma za kijamii kama zilivyokusudiwa ikiwemo kuboresha huduma za afya na miundombinu.
 
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege alisema mapato waliyopokea kutoka mgodi huo yako chini kwa shilingi milioni 300 ukilinganisha na kipindi kilichopita cha kuanzia Mwezi Julai hadi Desemba 2016 ambapo mgodi huo ulipokea shilingi milioni 760.
 
“Sisi tumepokea mapato haya kama tunavyopkea mapato mengine tunayopata katika halmashauri zetu,mapato haya ni yako chini ukilinganisha na kipindi kilichopita,tunaambiwa mapato yamepungua kutokana na Makinikia ambapo sasa yamesimama,hii inaleta changamoto katika ukusanyaji wa mapato katika halmashauri yetu, tunaamini mazungumzo baina Acacia na serikali yakiisha halmashauri yetu itapata mapato mengi Zaidi,” aliongeza Berege.
Hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 iliyotolewa na Mgodi wa Acacia Bulyanhulu kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akizungumza wakati wa kukabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala wilayani Kahama  jana Jumatano Julai 26,2017 katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kahama.Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu.
 Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (kulia) akishikana mkono na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew wakati wa zoezi la kukabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala hundi yenye thamani ya Shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akizungumza wakati akimkabidhi hundi hiyo Kaimu Mweka Hazina wa halmashauri hiyo Saleh Bugege (kushoto). Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Acacia Bulyanhulu Sarah Ezra Terry.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akizungumza baada ya kupokea hundi yenye thamani ya shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi yenye thamani ya shilingi milioni 460 kwa ajili ya ushuru wa Huduma kwa halmashauri ya Msalala.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Video:Wakili wa Lissu, Fatma Karume baada ya dhamana:Lissu ni shujaa.

Mahakama ya Kisutu imempa dhamana Mhe Tundu Lissu kwa sharti la kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana yenye thamani ya Shilingi milioni kumi, uamuzi uliotolewa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Rais Magufuli Awasili Jijini Dar. Awahutubia Wananchi Wa Tegeta Kwa Ndevu.

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, baada ya wananchi hao kusimamisha msafara wake alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017.
Sehemu ya wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, wakimsikiliza Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliposimama kuzungumza nao, alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017.
Sehemu ya wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, wakimshangilia Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliposimama kuzungumza nao, alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017. PICHA NA IKULU.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Ufafanuzi wa serikali kuhusu ajira 3,152 zilizotangazwa.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

TAFITI: Wanaosoma Habari Mitandaoni Hupoteza Kumbukumbu Haraka Kuliko Magazetini.

Kama wewe ni mfuatiliaji na msomaji wa habari mitandaoni basi bila shaka huenda ulishawahi kukumbana na hali ya kusoma habari ambayo baada ya kumaliza ukaanza kukumbuka kama ulishawahi kusoma habari hiyo sehemu fulani lakini umesahau, basi utakuwa upo sahihi kabisa.



Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na muandishi wa habari mkongwe wa Gazeti la Financial Times,  Michael Skapinker amebaini kuwa wasomaji wa habari mitandaoni wengi wao hupoteza kumbukumbu ya kuhifadhi habari walizosoma kwa muda mfupi sana ukilinganisha na wale wanaosoma habari kupitia Magazeti.

Mwandishi huyo amesema asilimia kubwa ya wasomaji wa habari mitandaoni hufikiria zaidi kutoa maoni na kushare habari walizozipenda na sio kutilia maanani kwenye usomaji wa habari.

Utafiti huo uliofanyika kwenye nchi 60 tu umeonesha kuwa wasomaji wengi wa habari mitandaoni wanasoma habari nyingi kwa muda mfupi huku wakifanya shughuli nyingine kitu ambacho kinawafanya wakose umakini wa kuzingatia kile wanachokisoma tofauti kabisa na wale wanaosoma habari kwenye magazeti ambao hupaswa kupumzika kabisa ili kuweza kusoma gazeti.

Kwenye nchi 60 alizofanya utafiti huo, Michael Skapinker amesema kuwa asilimia 85 ya vijana chini ya miaka 40 ndiyo wanaopendelea zaidi kusoma habari za mitandaoni huku 15% wakisoma habari kupitia Majarida na Magazeti.

Hata hivyo utafiti huo umeonesha ingawaje vijana wengi wanasoma habari mitandaoni ila ni wepesi sana kusahau habari walizoma yaani kupoteza kumbukumbu kwa muda mfupi ukilinganisha na wale wanaosoma habari kwenye Magazeti.

Utafiti huo pia umeonesha kuwa ingawaje kuna ongezeko kubwa la wasomaji wengi wa habari mitandaoni lakini bado kuna kundi la wasomaji hawaamini habari hizo mpaka wazikute kwenye magazeti.

Bwana Skapinker amesema ingawaje wasomaji wa mtandaoni hupoteza kumbukumbu haraka lakini bado watu wengi huvutiwa na habari za mitandaoni kutokana na uharaka wa kuzipata, kuokoa muda, kupunguza gharama na urahisi wa kutoa maoni ya walichokisoma.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

RC Gambo Ampa Onyo Godbless Lema.

Wakati Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema akisema haogopi kusema ukweli, Mkuu wa mkoa huo, Mrisho Gambo amemtahadharisha kuwa hataacha kumchukulia hatua iwapo atamtukana Rais John Magufuli na Serikali yake.

Lema ambaye ameanza kufanya mikutano ya hadhara katika jimbo lake jana kwenye Soko Kuu la Arusha mjini alisema haogopi kusema ukweli hata kama akipingwa na baba yake mzazi.

“Taifa lipo kwenye mgawanyiko mkubwa, wakuu wa wilaya na mikoa wanafanya maamuzi kwa maelekezo kutoka ngazi za juu,” alisema.

Aliongeza kuwa hali ya demokrasia nchini ni mbaya kwa kuwa hakuna usawa na kuwataka viongozi kuomba hekima wanapopata mamlaka ya uongozi.

Kadhalika amezungumzia hatua ya kujiuzulu kwa Diwani wa Muriet, Credo Kifukwe akisema kuwa Chadema haihitaji jeshi la watu wengi bali la wachache wenye umoja. 
“Nimeteswa sana katika mji wa Arusha, lakini nawataka wafuasi wa Chadema msilipize kisasi kwa wanaohama chama. Leo wapinzani hawaruhusiwi kufanya siasa, lakini Rais anazunguka nchi nzima,” alisema.

Mbunge huyo alisema Tanzania inahitaji demokrasia ya kweli na amani ya nchi haiwezi kutunzwa na polisi isipokuwa kwa upendo wa Watanzania.

Pia, alimtaka Gambo kujipanga wakati wa uchaguzi mdogo wa madiwani kwa kuwa Chadema imejipanga kikamilifu. 
Katika mkutano huo, Lema aliwapandisha jukwaani madiwani wawili wa Chadema jijini Arusha, Obeid Meng’roriki wa Kata ya Terat na Ruben Ngowi wa Kimandolu huku akisema amesikia wanataka kujiuzulu nyadhifa zao.

Hata hivyo, madiwani hao waliposimama walisema wao hawana bei ya kuweza kununuliwa na mtu yeyote.

Wakati Lema akiyasema hayo, Gambo alisema Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua katika utendaji wake, hivyo mwanasiasa yeyote hataruhusiwa kutoa matamshi yenye kumdhihaki Rais na Serikali.

Akizungumza katika mkutano na viongozi wa madhehebu ya dini uliofanyika jana kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC alisema: “Tumempa mbunge wa jimbo hili (Arusha Mjini) kibali cha kufanya mikutano na wananchi wake kwa sababu ni kiongozi aliyechaguliwa na wananchi, hatuna sababu ya kumzuia, ila hatutakubali kusikia kwenye mikutano yake akimtukana Rais wetu na Serikali yake. Akifanya hivyo tutamshughulikia.”

“Mtu yeyote anayetaka kuichezea Serikali na kutaka kukwamisha ajenda zake tutawang’oa iwe kwa greda au kwa namna nyingine yoyote, Rais Magufuli alipita nchi nzima akitoa ahadi zake na wamemchagua sasa wamwache atekeleze alichowaahidi wananchi.”

Gambo alitumia mkutano huo kuzungumzia kadhia ya rambirambi zilizotolewa kufuatia ajali ya wanafunzi wa Lucky Vincent iliyopoteza maisha ya watoto na wafanyakazi wapatao 35 na baadaye Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro na Lema kutilia shaka matumizi yake.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

Utofauti kati Ya Mwanamke na Mwanaume Katika Hisia Za Kimapenzi.

Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia inasadikika hakuna kitu ambacho kina nguvu sana kama mahusiano ya mapenzi, hata hivyo kutokana na nguvu hiyo ya mahusino, watu wengi husaani mwanaume ndio ambao wanaathiriwa kwa kiwango kiubwa na nguvu hiyo.

Watafiti wa masuala ya mahusiano wanazidi kusema ya kwamba, mwanaume kila baada ya dakika tano ni lazima awaze masuala ya kimapenzi, hii ni kutokana wanaume wengi hupenda zaidi jinsia ya kike kwa kuona kwa macho. Ndo maana ukichunguza kwa makini wanaume huwa wanakuwa wanazingatia zaidi katika kutazama jinsia hii ya kike mahali popote walipo.

Hivi hujawahi ona wanaume wamekaa mahali wanapiga stori ghafla akapite mwanamke mzuri mbele ya macho yao ghafla stori zile zikasimama kwa muda? Bila shaka umewahi kuona. Utawasikia wakisema kwa minong'ono aaah angalia kifaa hicho, wapo wengine utawasikia wakisema mcheki chura huyo. Hii ina maana ya kwamba macho ya mwanaume ndio chanzo kikubwa cha kuingia katika mahusiano kabla ya kumjua tabia aliyonayo mtu huyo.

Lakini ukweli ambao upo nyuma ya pazia ni kwamba wanaume wengi  huingia katika matamanio ya kimahusiono kwa kuona kwa macho zaidi tofauti na mwanamke. Hata hivyo mahusiano ya kimapenzi aliyonayo mwanaume ni matokeo ya macho yako. Kwa maneno mengine tunaweza kusema matamanio ya hisia za mwanamke yapo katika kuona zaidi kuliko kitu chichote.

Lakini ukienda upande wa pili wa shilingi, mwanamke huwa yupo tofauti sana ukilinganisha na mwanaume katika suala zima la kuingia katika mahusiano. Hisia za mwanamke huwa zipo zaidi katika maneno na mguso katoka kwa mwanaume. Hisia za mwanamke huwa hazipo katika kuona kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na mwanaume.

Mwanamke huamini sana katika maneno ambayo ataambiwa na mwanaume,  kwa mfano mwanamke akiambiwa anapendwa zaidi ya kitu chochote katika dunia hii mwanamke huamini hivyo,hivyo maneno ya mwanaume yana nafasi kubwa katika kuziteka hisia za mwabamke.

Lakini pia kama hiyo haitoshi mwanamke hupata hisia zaidi pale anapoguswa na mwanaume, hivyo ndo maana kama utakutana na msichana kwa mara ya kwanza atakaa usimguse katika mwili wake, hii ina maana mguso wa mwanaume una nguvu sana katika kuamsha hisia mwili wa mwanamke.

Hivyo kama ndivyo hivyo basi hii ni uofauti mkubwa ulipo kati ya mwanaume na mwanamke katika kuamsha hisia za kimapenzi. Na kitu kikubwa ambacho huongoza hamasa na kudumu katika mahusiona ya kimapenzi ni "mawasiliano" , mawasiliano ndiyo chachu kubwa katika mahusiano yenu. Hivyo kila wakati ili muweze kudumu katika mahusiano yenu hakikiasha unakuwa na mawasilino bora kati yako na mwenzi wako.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

TEGETE AFURAHIA KUTUA MAJIMAJI, ASEMA ANATAKA KUREJESHA MAMBO YAKE.

Jerry Tegete ameonyesha kufurahia kusajiliwa Majimaji ya Songea.

Tegete amesema anaamini Majimaji inakuwa maisha yake mapya ya soka na anatamani kufanya vema.

“Maisha ya soka haujui utaenda wapi, lakini ninataka kurudisha kiwango changu na kufanya vizuri zaidi nikiwa na Majimaji,” alisema.


Tegete ameondoka Mwadui FC na kujiunga na Majimaji ambaye msimu uliopita ilifanya kazi ya ziada kujikomboa isiteremke daraja.

Tegete alikuwa kinara katika ufungaji wakati akiichezea Yanga.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa

FLORA Mbasha na Emmanuel Mbasha Watakiwa Kuacha Utoto...Kisa Kizima Hichi Hapa.

Hakuna kazi ngumu kama kutoa ushauri kwa watu wenye mgogoro unaohusisha uhusiano wa kimapenzi, kwa sababu ni lazima upande mmoja utachukia, kwani ili kitu kiwe kizuri, ni lazima uwe mkweli kwa asilimia mia moja.

Ni lazima mmoja atachukia kwa sababu siku zote katika uhusiano wa kimapenzi, upande mmoja unakosea.

Barua yangu ya leo inawaelekea kaka na dada yangu, Emmanuel Mbasha na aliyekuwa mkewe, Flora, siku hizi akifahamika kama Madam Flora.

Dada yangu Flora, ninamkubali tangu alipoanza kufanya vyema na Wimbo wa Jipe Moyo, Majaribu na nyinginezo.

Dada Flora, wewe ni mtumishi wa Mungu, kama unaamini kuwa majaribu ni kipimo kwa mtu aliyeokoka, kwa nini unashindwa kumaliza bifu lenu kimya kimya ukizingatia kila mtu kwa sasa ana maisha yake mapya?

Hii ni kwa sababu ya ule unaodaiwa kuwa ujumbe wako kusambaa ambao ulimsema vibaya mumeo wa zamani, kwamba alikuwa chanzo cha kuachana kwenu.

Pengine maisha ya kistaa yamewaathiri au labda huenda bado mnapendana, lakini mbona mnafanya kama hili jambo la kutengana mmelianzisha nyinyi? Nasema hivi kwa sababu migogoro katika ndoa haijaanza leo na wala haitakwisha kesho, ni vitu vya kawaida ambavyo binadamu hupitia.
Sasa kama ilitokea kama ilivyotokea, kuna haja gani ya kupeana vijembe kila kukicha kana kwamba mnashindana kupata tuzo?

Maana kama mmeshindwana na kila mtu ana maisha yake, ya nini kuanza kufukunyua mambo ya faragha kwa watu ambao hawakuwepo huko?

Huko ni kujishushia heshima kwa wote, kwani wewe na mwenzio, mnatambulika kama Watumishi wa Mungu, wapo kondoo wengi ambao walikuwa wanapenda kuiga mfano wenu kama waimbaji na hata wanandoa.

Mmeachana basi, udhaifu na changamoto mlizopitia kwenye ndoa yenu zibaki mioyoni mwenu.
Ndoa yenu imefika mwisho, walimwengu wote wanajua hilo lakini mnapoanza kuchafuana mitandaoni, sidhani kama ni sahihi. Najaribu kuitafuta hekima ya Mungu kati yenu, siioni! Najaribu kujiuliza, mnachafuana kwa sababu ya uwepo wa mitandao ya kijamii au hata kama isingekuwepo mngefanya hivyo?

Kama ni ndoa kuvunjika yenu si ya kwanza, kama ni wanandoa kutibuana na kulumbana, nyinyi si wa kwanza, kama ni migogoro ya kwenye ndoa hata wazazi wetu wameipitia, lakini mbona sababu za mizozo yao hatuijui?

Kinachosikitisha ni kuona kaka Emma naye kaja kujibu mashambulizi kwa maneno makali na yenye vijembe ndani yake. Ingawa hakumtaja mwenzake moja kwa moja, lakini wanaojua fukuto hilo wanajua ndiyo maana vyombo vya habari vimeripoti.

Kaka Emma, mbona ndoa nyingi zina mifarakano mingi sana, mbona wanandoa wengi wameachana lakini wamebaki na vidonda vyao moyoni, si kila jambo la kujibu.

Wakati mwingine ili uonekane una hekima ni vyema ukapotezea tu kuliko kuanza kuandika maneno yanayoondoa hekima, uvumilivu, burasa na utashi wa Kimungu ndani yenu.

Wapo watu wengi ambao wamevunja ndoa zao na kila mtu akawa na maisha yake na wanasalimiana na kupendana kama watu wa kawaida, lakini kwa hiki ninachokiona kwenu si jambo jema, hakuna sababu ya kujengeana uhasama wakati mlioana ili mfurahie maisha lakini kwa kile kilichotokea basi kila mtu afanye yake kwa moyo mweupe.

Vinginevyo ni kama mnatafuta promo ili watu wajue uwepo wenu. Kuna njia nyingi nzuri na zenye mbolea zinazoweza kuwafanya muonekane mbele za watu, kama kufanya kazi yetu na kumtukuza Mungu kupitia nyimbo za Injili au hata kuwapa chochote watoto yatima au watu wenye uhitaji.
Haya mambo mnayofanya waachieni watoto wadogo wa Bongo Fleva wanaoamini kiki ndizo zitawapandisha badala ya kufanya kazi kwa bidii.

GABRIEL NG’OSHA | BARUA NZITO
Maoni & Ushauri:
+255 620 744 592
GPL

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa