STAA wa sinema za Nigeria (Nollywood), Ramsey Nouah amewalipua waigizaji wa filamu za Kibongo kwa kushindwa kuendeleza sanaa hiyo kwa kiwango alichoishia marehemu Steven Kanumba huku akilizungumzia kaburi la staa huyo, Ijumaa Wikienda lina mkada kamili.
Unapozungumzia Bongo Movies unawagusa vinara wake, Vincet Kigosi ‘Ray’, Wema Isaac Sepetu, Kajala Masanja, Aunt Ezekiel, Jacob Steven ‘JB’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wengine wengi waliofanya kazi na Kanumba.
Katika Makaburi ya Kinondoni, Dar alikozikwa Kanumba miaka mitano iliyopita, Ramsey ambaye kwa mara ya kwanza alifika kaburini hapo wikiendi iliyopita alionekana mwenye huzuni kubwa na kushindwa kujizuia ambapo alimwaga machozi mfululizo kabla ya kutamka maneno mazito yaliyosisimua wengi waliofika kaburini hapo.
Mama Kanumba akilia kaburini kwa mwanaye.
MAMA KANUMBA
Muda mfupi baada ya kuwasili makaburini hapo, Ramsey alimshika mkono mama mzazi wa Kanumba, Flora Mtegoa na kumkumbatia na ndipo vilio vikashika nafasi hususan kwa mama huyo.
MAOMBI
Ramsey, alitumia dakika chache akiwa kimya huku uso wake ukionesha maumivu na ghafla alianza kushusha maombi akimuombea marehemu Kanumba huku watu wote wakimsikiliza.
“Baba, utukufu wako ni wa kipekee tazama tumesimama hapa leo tukiwa na huzuni mioyoni mwetu, machozi yakighubika mboni za macho yetu tukimkabidhi kwako mja wako, Steven (Kanumba) aliyelala hapa kwa mapenzi yako, mpokee mwanao baba na kumsamehe dhambi zake ili siku moja tuonane naye kwa mapenzi yako yakitimizwa, baba tazama moyo wangu ulivyokwazwa na kifo hiki, hakika sitaki kukufuru, lakini ulimchukua Steven wakati dunia ikimhitaji zaidi, lakini jina lako lihimidiwe kwa kila jambo,” aliomba Ramsey.
Baada ya kumaliza maombi hayo, Ramsey alianza kuzungumza maneno ambayo yaliashiria alikuwa akimwambia Kanumba, jambo lililoshangaza na kuvutia watu waliokuwepo.
“Steve, nimesimama mbele yako leo ukiwa hujitambui. Tuliachana ukiwa na pumzi yako, lakini leo (Jumamosi iliyopita) niko kando ya mahali ulipolala na huwezi kuamka japo kunipa mkono, lakini kibaya zaidi hukuniambia maneno ya kwaheri, kwa nini hukuniaga Steven? Kuna mahali nilikukosea?
Aaah nashindwa kuhimili maumivu haya, ninalo kaa la moto kifuani mwangu, lakini kinachoniumiza zaidi ni kwamba mahali ulipolala hapaendani na hadhi yako, hukupewa kabisa thamani yako kulingana na ulichokifanya kwenye tasnia ya filamu na bila kuficha ni kwamba filamu za Kitanzania zinakufa, najua huko uliko unaumia na kinachoendelea kwenye filamu zanu,” alisema Ramsey katika ‘mazungumzo’ yake na Kanumba.
Baada ya kumalizana na ibada ya kaburini kwa Kanumba, Ramsey alizungumza na waandishi wa habari na kulipuka maneno ambayo yalilenga kuwananga waigizaji wa filamu za Kibongo.
“Ni ukweli ulio wazi kwamba filamu za hapa (Bongo) zimekosa msisimko, lakini wanayo nafasi ya kurekebisha, nimesimama hapa na maumivu makali, lakini yote ninamshukuru Mungu na wito wangu kwa wasanii wamsaidie mama huyu (mama Kanumba) kwani mwanaye alitoa ajira kwa wasanii, lakini leo wanamuona mama huyo kama si chochote, wameshindwa kumuenzi Steven kulingana na thamani yake, waangalie mahali walipokosea ili laana ya Steven isizidishe makali yake, lakini kubwa wamsaidie mama huyu,” alisema Ramsey akipeleka ujumbe huo kwa wasanii wa Bongo Movies.
KUHUSU LULU
Katika mazungumzo hayo, Ramsey hakutaka kuingia kwa undani kuhusiana na msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye kwa sasa yuko jela akitumikia kifungo cha miaka 2 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia Kanumba, April 7, 2012 nyumbani kwa jamaa huyo, Sinza- Vatican, Dar.
Chanzo: Global Publishers
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment