Home »
Habari Moto
» Abiria wamiminika Ubungo Daradara Zaruhusiwa Kwenda Moshi, Arusha.
Magari ya abiria (daladala) yameanza kutumika kupakia abiria wanaosafiri kwenda mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ili kupunguza adha ya usafiri kwa abiria wanaosafiri msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.Akizungumza na Mwananchi, leo Jumanne Desemba 19, Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani Ubungo (UBT),Inspekta Swamix Ibrahimu amesema gari hizo zimeanza kubeba abiria na asubuhi ya leo daladala nne zimeondoka kuelekea Moshi na Arusha."Daladala unazoziona hapa, tunazikagua na zipo kwaajili ya dharura endapo itatokea abiria wakawa wengi basi tunaruhusu zinapakia "amesema.Si kwamba zinapakia muda wowote, hapana tutakuwa na daladala tano kwa siku ambazo zinakuwepo ikitokea abiria wameongezeka na basi kubwa hakuna basi tunaruhusu" amesema Ibrahimu amesema abiria bado hawajawa wengi kiasi cha kuruhusu daladala nyingi kupakia. Mmoja wa wasimamizi wa daladala ambazo zimekutwa zikikaguliwa, Ignas Swai amesema gari zake ni imara na tayari zimekaguliwa na Askari na kupewa kibali na Sumatra."Nauli tunatumia IleIle iliyowekwa na Sumatra na tunapakia abiria wanaoenda Moshi na Arusha "amesema.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
Related Posts:
Raila Odinga Apuuza Kauli ya Serikali...Adai Kuapishwa Kwake ni Alali.
Kiongozi wa Muungano wa Upinzani (NASA), Raila Odinga amejitokeza katika viwanja vya Uhuru na kuapishwa kama Rais wa Watu wa Kenya.-Viongozi wengine wa Muungano huo, wakiwemo Kalonzo Musyoka, amabye ndiye alitarajiwa kuapa … Read More
Zitto Ataja List ya Viongozi Ambao Atawateua Ikitokea Amekuwa Rais wa TZ.
Mchana wa leo January 30, 2018 kwenye ukurasa wa mtandao wa Twitter wa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika watu ambao atawateua kushika nyadhifa mbalimbali za serikali kama atakuwa Rais wa Tanzania.Ameandika kuwa a… Read More
Rais Magufuli Kuzindua Pasipoti ya Kielektroniki.
Jonas Kamaleki- MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli leo
atazindua Pasipoti Mpya ya Tanzania ya kielektroniki jijini Dar es
Salaam.
Uzinduzi huo utafanyika Jumatano, Januari 31, … Read More
Kimenuka Kenya...Raila Odinga Hatarini Kushtakiwa kwa Uhaini.
MAMLAKA za Kenya, jana zilizima vituo vya televisheni kuzuia matangazo
'live' ya sherehe za kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga,
ambaye alisusia uchaguzi wa marudio wa mwaka jana uliobishaniwa.
Alijitangaza … Read More
Maskini...Familia Yahofia Tundu Lissu Kufukuzwa Hospitali.
Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), imelitaka
Bunge kutoa fedha za matibabu yake kama halitaki mtunga sheria wake
huyo akafukuzwe hospitalini alikolazwa.
Lissu amelazwa katika Hospitali ya Chuo… Read More
0 comments:
Post a Comment