Tuesday, 2 May 2017

Cristiano Ronaldo apiga Hat-trick mbele ya Atletico Madrid.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa  
 

Serengeti boys sasa yapangiwa kundi B Libreville.

Timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys, imebadilishiwa kituo kutoka Port Gentil na sasa imepangiwa Libreville.
Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Niger, Angola na Mali ambako watafungua nayo mchezo Mei 15, mwaka huu. Kwa mabadiliko hayo, Kundi A lenye timu za Cameroon, Ghana, Guinea pamoja na wenyeji Gabon, litakuwa Port Gentil.

Kwa sasa Serengeti Boys wako Cameroon kwa kambi ya wiki moja iliyoanza Aprili 29, mwaka huu ambako tayari imecheza na wenyeji Cameroon mchezo mmoja na kushinda bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika jijini Yauonde.

Wenyeji hao, Cameroon watarudiana na Serengeti Boys katika mchezo mwingine wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kesho Jumatano, Mei 3, mwaka huu.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

MAREKANI Waanza Upya Kuichokonoa Korea Kaskazini..Watuma Ndege za Kivita Kufanya Mazoezi Mpakani Mwa Nchi Hiyo.

Maafisa wa Korea Kusini wamesema ndege mbili za Marekani za kuangusha mabomu zimepaa juu ya anga la rasi ya Korea.
Ndege hizo za kivita zilipaa angani kama sehemu ya juhudi za kuzuia vitisho na uchokozi kutoka kwa Korea Kaskazini.
Ndege hizo aina ya B1-B zilishiriki operesheni ya pamoja na ndege za kivita za Korea Kusini.
Kupaa kwa ndege hizo kumetokea wakati ambapo Rais Trump ametoa taarifa za kukanganya kuhusu msimamo na sera ya Marekani dhidi ya Pyongyang.
Bw Trump aliambia Fox News kwamba msimamo wa Korea Kaskazini kuhusu mpango waker wa kufanyia majaribio makombora ya nyuklia ni wa kukera.
Alikuwa awali amesema kwamba yuko tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un, iwapo kutakuwepo na mazingira mahsusi.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

NYOTA ya Mbwana Samatta Yazidi Kuwaka..Shabiki Ingia Uwanjani na Bango la Kuomba Jezi yake.

Ukisema mambo yanaanza kunyooka, baada ya mashabiki wengi wa KRC Genk kuonyesha imani kubwa kwa mshambulizi, Mbwana Samatta.

Samatta anaonekana kuwa bora zaidi kutokana na kuwa tegemeo katika kikosi cha Genk cha Ubelgiji.
Imeonekana mmoja wa shabiki akiwa na bango uwanjani, akiomba jezi ya Samatta..!!!

Tupia neno lolote kwa Samatta kama ishara ya kumtakia kila la kheri katika soka...!!!
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

VIDEO MPANGAJI AMCHOMA KISU MPANGAJI MWENZAKE KISA KIZIMA HIKI HAPA.

May 2, 2017 kupitia Heka heka ya Leo Tena ya Clouds FM mtangazaji Geah Habibu ametuletea hii stori iliyotokea Kiwalani ambako mpangaji mmoja kuchomwa kisu na mpangaji mwenzake kisa kikiwa ni ndala.

Inadaiwa kuwa mpangaji huyo alikuwa kwa masharti kwa wapangaji wenzake akiwaambia kuwa hataki mazoea na mtu na kuwaonya kuwa hata familia yake pia wasiizoee.

Kisa cha kumchoma kisu mpangaji mwenzake ni kwa sababu ya ndala za mpangaji mwingine kuvaliwa na mgeni wake hivyo kuzua vurugu zilizopelekea wawili hao kuzozana



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

HIMID Mao Akwea Pipa Kwenda Denmark kwa Majaribio Katika Klabu ya Randers FC.

Mchezaji wa klabu ya Azam FC na Taifa Stars, Kiungo Himid Mao amekwea pipa jana jioni akielekea nchini Denmark, kwa ajili ya majaribio ya kutafuta kucheza soka la kulipwa katika bara la Ulaya.
Kiungo huyo machachari anakwenda kufanya majaribio yake ya soka la kulipwa katika klabu ya Randers FC ambayo iko katika ligi kuu nchini Denmark maarufu kwa jina la Superliga.
Mao amekuwa katika kiwango cha juu katika ligi ya msimu huu pamoja na michuano mingine ambayo kiungo huyo amekua akicheza.
Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amethibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo akisema, “Tuna wachezaji zaidi ya sita wameenda ulaya kwa majaribio, na Mao ni mmoja wao. Taarifa zingine tutatoa kama klabu ila Mao ana baraka zote za klabu kuondoka. 
Amepata nafasi ya kuondoka, na hakuna atakaemzuia, wote wataondoka na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu wote tunaamini watafanikiwa na wataweza kuanza maisha mapya katika nchi moja wapo,”


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

LISSU Ataja Adui wa Wafanyakazi.

RAIS wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Tundu Lissu, amesema Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (Tucta) ndiye adui wa kwanza kwa wafanyakazi.
Lissu ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Nishati na Madini nchini (NUMET) katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mjini hapa.
Alisema Shirikisho hilo ni mwiba kwa wafanyakazi kutokana na kushindwa kusimamia haki za wafanyafakazi kama inavyotarajiwa, badala yake linashirikiana na Serikali kuwanyanyasa.
Kutokana na hali hiyo, Lissu aliwataka wafanyakazi kubadilika katika mitazamo yao ili waweze kudai haki zao na siyo kuziomba kama wanavyo fanya hivi sasa.
“Wafanyakazi badilikeni, haki haiombwi bali inatafutwa, inadaiwa hata ukiona nchi ambazo wafanyakazi wake wanapata raha leo hii walipambana hata kumwaga damu kwa ajili ya kupata haki zao za msingi, acheni kuwa ombaomba wa haki zenu,” alisema.
Alisema ni vigumu kwa wafanyakazi kuomba haki zao kwa watu ambao wamewatesa kwa zaidi ya miaka 50 kwa kuwalipa mishara midogo ambayo pia imekuwa ikikatwa kodi kubwa.
“Wafanyakazo wadogo leo hii wanahangaika na wanahitaji unafuu maana wanakatwa kodi ambayo hupunguza mishahara yao wakati wengine hawatoi hata senti tano katika kodi hali hii inafanya ubaguzi wa hali ya juu,” alisema Lissu.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa NUMET, Nicodemus Kajungu, alisema kuna haja ya kuundwa wa shirikisho lingine la vyama vya wafanyakazi nchini kutokana na kuonekana kuwa Tucta inawatenga.
“Leo hii sisi vyama ambavyo sio wanachama wa Tucta tumenyimwa nafasi ya kushiriki kule Moshi, hivyo basi ipo haja ya kuwa na shirikisho letu ambalo litasimamia kwa nguvu zote haki zetu na kuboresha maslahi ya wafanyakazi na Tucta iendelee na wanachama wake 12 ilionao sasa,” alisema Kajungu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

CHAKULA cha Kuzuia Kuzeeka Haraka.

ILI kudumisha muonekano wa ujana kwa mwili wako unahitaji kuupa mahitaji yake yaliyobadilika. Kuzuia kuzeeka haraka unahitaji chakula chenye calcium ya kutosha kuipa mifupa yako nguvu na kupata chakula chenye collagen kwa wingi ili kuifanya ngozi yako isiwe na makunyanzi mwilini, kiashiria cha uzee.
Katika miaka ya 1950 Mmarekani mwanasayansi mtafiti, Denham Harman aligundua kuwepo uhusiano mkubwa kati ya mwili kuzeeka na uwepo wa kemikali ambazo hutengenezwa na mwili katika ufanyaji wake kazi wa kawaida katika mwili wa mtu, kitaalamu huitwa free radicals.
Mwili una uwezo wa kudhibiti madhara yanayotokana na uwepo wa free radicals kwa kiasi fulani, lakini idadi ikizidi mwili huzidiwa na madhara mengi hutokea, yakiwepo kuzeeka kwa mwili na magonjwa mengi kama kansa, magonjwa ya moyo, mifupa (arthritis), usahaulifu (Alzheimer’s), ugonjwa wa parkinson’s na kisukari.
Free radicals katika mwili huweza kuongezeka kwa kutumia vitu kutoka nje ya mwili. Sumu kutoka nje zinazozalisha free radicals katika mwili ni pamoja na hewa chafu hasa inayotoka kwenye viwanda, moshi wa sigara, na chakula chenye dawa za kuulia wadudu na utumiaji wa pombe kwa kiwango cha kuzidi kiwango.
Kiwango kidogo cha free radicals kinachozalishwa na mwili wenyewe kinaweza kikadhibitiwa vizuri na kemikali nyingine zinazoitwa antioxidants ambazo nazo pia huzalishwa na mwili.
Free radicals za ziada zinazozalishwa na vitu kutoka nje ya mwili zisipodhibitiwa kikamilifu husababisha madhara mengi pamoja na magonjwa yaliyotajwa hapo juu.
Hivyo basi tunahitaji kupata chakula chenye antioxidants kwa wingi ili kuisaidia miili yetu kupambana na kemikali hizi za ziada. Kuna aina nyingi za antioxidants zikiwemo vitamini C, vitamini E, flavonoids na polyphenols kwa kutaja tu bila kuingia kwa undani zaidi.
Baada ya utangulizi huo, sasa ni wakati wa kupitia chakula ambacho kikitumiwa kitakupa vitu tulivyovitaja hapo juu na kuufanya mwili wako kuwa na mwonekano wa ujana daima.
Vitamini C
Katika utafiti wa Mtafiti Herman uliofanywa kwenye kikundi cha wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya 40 ulionyesha kwamba wanawake wanaotumia chakula chenye vitamini C zaidi walikuwa na makunyanzi zaidi na ngozi zao hazikuwa kavu ukilinganisha na wale ambao walitumia vitamini hiyo kidogo.
Hii ni kwa sababu vitamini C ni antioxidant yenye nguvu inayozuia uharibifu wa seli na DNA za seli hivyo kulinda uzalishaji wa collagen ambayo ndiyo nguzo muhimu ya kulinda ngozi yako.Unashauriwa basi upate angalau miligram 75 za vitamini hii kwa siku.
Kwa mfano unaweza kupata chungwa moja wakati wa kifungua kinywa na pilipili tano za njano ndani ya saladi kwenye mlo wako wa mchana. Chakula chenye vitamini C kwa wingi ni broccoli, strawberries, pilipili nyekundu, nyanya, tikitimaji n.k.
Chakula chenye protini
Tafiti zilionyesha kuwa wanawake waliotumia protini zaidi walikuwa na makunyanzi machache zaidi kwenye ngozi zao kuliko wale ambao walitumia protini kidogo, hii kwa sababu protini hutoa viungo muhimu katika ujenzi wa collagen.
Ili upate protini unashauriwa kula nyama ya kuku isiyo na ngozi, sehemu nyeupe ya mayai na samaki. Unapochagua kula nyama ya ng’ombe au mbuzi, pendelea kutumia ile isiyo na mafuta. Matumizi ya soya yameonyesha kusaidia kuondoa ile mistari myembamba kweye macho.
Samaki
Samaki wa baharini wenye mafuta wamebainika kuwa na kiwango kikubwa cha ‘omega-3 fatty acids’, kitu ambacho husaidia kuilinda ngozi yako kutokana na mionzi mibaya ya jua ambayo hudhoofisha collagen.
Nafaka
Utumiaji wa nafaka zisizokobolewa badala ya wali mweupe, mikate inayotokana na ngano isiyokobolewa (brown bread) na nafaka nyingine una faida nyingi. Moja ni kuzuia mwongezeko wa insulin katika mwili ambayo ina madhara ya kuharibu ngozi. Pia nafaka nzima ni chanzo cha madini ya selenium ambayo husaidia kuikinga ngozi yako kutokana na mionzi ya jua.
Unashauriwa kutumia mchele usiokobolewa (brown rice), shayiri na ngano isiyokobolewa ili uweze kupata madini haya yatakayokusaidia kulinda ngozi yako.
Green Tea
Green tea ni kinywaji chenye antioxidants nyingi. Unywaji wa vikombe viwili au vitatu kwa siku vya chai hii utaifanya ngozi yako kuwa nyororo na kutopata makunyanzi.
Hatuwezi kuorodhesha vyakula vyote ambavyo vinafaa katika kuzuia kuzeeka haraka katika nafasi hii, hivyo makala yetu inatoa mwongozo tu wa kula.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

MAGUFULI Ageukia 'Waliofoji' Umri.

RAIS John Magufuli amesema serikali inawachunguza watumishi wa umma waliogushi umri ili wasibaki kwenye utumishi wa umma kwa muda ambao hawakustahili kuwa kazini.
Kadhalika, amesema kuna watumishi wenye miaka 60 na zaidi ambao hawataki kustaafu huku waking’ang’ania ajira na madaraka, na wengine wakijipachika vyeo vya ukurugenzi.
Akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) ambazo kitaifa zilifanyika jana katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Rais Magufuli alisema uchunguzi huo wa umri umeshaanza.
“Wako watumishi ambao wamebadilisha umri wao," alisema Rais Magufuli. "Wamebadilisha miaka yao na unakuta ni mzee kabisa, lakini kabadilisha umri."
"Kuna watu ambao ni wazee tena kuliko mimi. Wanasema hawaondoki eti ndio wakati umefika, hao nao tunawachunguza.”
Katika hotuba yake, Rais Magufuli alisisitiza kuwa wapo watumishi wa umma ambao bado wanafanya kazi wakiwa wameshatimiza umri wa kustaafu kwa lazima wa miaka 60 lakini hawataki kustaafu ili kuachia nafasi wegine waajiriwe.
Uchunguzi huo unakuja siku chache baada ya serikali kufanya uhakiki wa vyeti vya elimu vya wafanyakazi wake na kugundua takriban watumishi 10,000 wana vyeti vya kughushi. Wamefukuzwa kazi mara moja.
Akionyesha kukerwa na hali hiyo Rais Magufuli alisema:
“Sheria za nchi yetu hazijasema mtu anayetakiwa kufanya kazi lazima awe na digrii, kila kazi ina qualification (sifa) zake.
"Haiwezekani Watanzania wote wakawa na digrii, darasa la saba wanaajiriwa, form four (kidato cha nne) wanaajiriwa na wenye certificate (cheti) wanaajiriwa.
"Na kila mmoja ana wajibu wa kuajiriwa.
”Tunachosisitiza hapa kama wewe ni darasa la saba na unataka kuajiriwa kaombe kazi ya darasa la saba, kama wewe ni form four kaombe kazi ya form four, kama una certificate nenda ukaombe kazi ya certificate. Usiende ukatafute mavyeti ya kufoji ukajiita daktari kumbe hata unesi haujafikia,”alisema
Aidha, Rais Magufuli alisema wako watumishi ambao wamekuwa wakijiita wakurugenzi, "watu wakubwa wakubwa tu, wana mavyeti ya kufoji, halafu wanawanyanyasa hawa watu wa chini ambao wana vyeti halali."
Alisema kundi hilo nalo ni miongoni mwa watumishi wa umma ambao serikali imekuwa ikiwaamini lakini imegundua kumbe hawastahili nafasi hiyo.
Mbali na kuahidi kushughulikia watumishi walioghushi umri ili kufanya kazi nje ya miaka ya kustaafu, Rais Magufuli alistahili kurejesha nyongeza ya kila mwaka ya mishahara na upadishaji watumishi madaraja.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

FAHAMU Njia za Mkato Zinavyoweza Kukupa Mafanikio Yenye Uchungu.

NDUGU zangu, linapokuja suala la kutafuta maisha mazuri na yenye mafanikio, wapo watu ambao wanadiriki kujiingiza katika shughuli zisizo halali ambazo mwisho wa siku zinaweza kuyahatarisha maisha yao.
Lakini niwakumbushe tu kwamba, zipo kazi nyingi tu ambazo ukizifanya kwa nguvu zote na kwa malengo unaweza kuwa na mafanikio makubwa na ukaishi maisha ya furaha na amani. Hapa nazungumzia zile kazi ambazo ni halali.
Lakini huwa najiuliza, hawa wanaofanya kazi zisizo halali walishawahi kujiuliza hatima ya maisha yao itakuwaje?
Kwa nini ufi kie hatua ya kufanya kazi ambayo itafanya maisha yako yawe hatarini? Wapo wanaosema eti wanafanya hivyo kwa sababu maisha ya sasa ni magumu na hivyo ugumu huo wa maisha unaweza kuukabili kwa kufanya kazi hizo.
Hii ni hatari sana na hata hao wanaojipatia mapesa kwa kufanya kazi kama vile za kuuza madawa ya kulevya, bangi, utapeli, uchangudoa na shughuli nyingine za namna hiyo maisha yao si ya furaha kama watu wanavyodhani. Wanaishi maisha ya wasiwasi huku wakihofi a usalama wa maisha yao.
Uchunguzi unaonesha kwamba wengi wanaofanya biashara hizo haramu mwisho wao huwa mbaya sana ambapo baadhi yao huishia kuuawa, kufa ama kufungwa jela.
Nenda kwenye magereza leo hii utakuta waliojaa huko wanatuhumiwa kwa ujambazi, wizi, uuzaji wa madawa ya kulevya, watu ambao walidhani kwa kufanya hivyo wanaweza kuyafanya maisha yao yakawa mazuri kumbe ndiyo wanajiweka katika wakati mgumu zaidi.
Mimi nadhani zipo kazi nyingi tu ambazo unaweza kuzifanya na ukawa tajiri ama kuwa na mafanikio makubwa bila kuiba kitu cha mtu wala kudhulumu. Kwa kutumia akili yako, nguvu zako pamoja na maarifa aliyokujaalia Mungu naamini unaweza kufanikiwa na kuishi maisha ya amani yaliyojaa furaha tele.
Siyo mpaka uibe ndiyo unaweza kufanikiwa, siyo lazima uuze madawa ya  kulevya wala kuuza mwili wako ndiyo ufanikiwe. Fahamu kwamba wapo watu wengi waliopata mafanikio makubwa kwa kupigana kihalali.
Hivi unadhani watu mabilionea na wenye mafanikiio makubwa duniani
walifi kia hatua hiyo kwa njia za mkato? La hasha! Hao walitumia akili na nguvu zao katika kuusaka utajiri huo.
Siku zote ukae ukijua kwamba maisha hayana njia ya mkato. Kwa maana hiyo basi wanaoendesha maisha yao kwa njia ya mkato, hawana furaha na mafanikio ya kweli katika maisha yao.
Kimsingi wanaotegemea kuendesha maisha yao kwa kufanya kazi ambazo siyo halali wako kwenye nafasi nzuri ya kukumbwa na balaa katika maisha yao kiasi cha kuwafanya kutozifurahia fedha walizonazo.
Wapo akina dada ambao wameridhika kuendesha maisha yao kwa kufanya biashara ya kuuza miili yao. Wanaofanya hivyo wanaeleza kwamba kinachowasukuma kufanya hivyo ni ugumu wa maisha.
Maisha yanaweza kuwa magumu kama hutajishughulisha.
Lakini hata kama maisha ni magumu kiasi gani ndiyo ufi kie hatua ya kuweka rehani maisha yako?
Asikudanganye mtu wengi wanaofanya biashara ya uchangudoa maisha yao yako hatarini hasa kipindi hiki ambacho ugonjwa wa Ukimwi unasumbua kila kona ya ulimwengu.
Labda nihitimishe kwa kusema kwamba, kuna kila sababu ya kubadilika na kuangalia njia sahihi za kuendesha maisha yetu. Tuachane na tamaa zisizo na msingi na kutaka kujipatia fedha kwa njia za makato. Tuelewe kwa kufanya hivyo hatuwezi kupata mafanikio ya kweli na tutakuwa tunayahatarisha maisha yetu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

MBUNGE Kingu Awafungukia Wanaodai Anatoka Kimapenzi na Mwanamuziki Vanessa Mdee.

Unakumbuka story ya Vanessa Mdee Kutoka na Mbunge????...


Mbunge Afunguka haya:

"Hekima na utulivu wako vinadhihirisha kuwa umekomaa.walimwengu sio wazuri hukumu yao ni batili lakini siwezi kuacha kujali kuwa ur my close friend na una nidhamu na heshima acha wahukumu wajuavyo ila ninakupenda kama mtu wa karibu na rafiki wa kuamimi. ."
.
.
TOA MAONI YAKO HAPA -


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

Aslay Ft. Khadija Kopa (Video) – Usiitie Doa.

Aslay Ft. Khadija Kopa (Video) – Usiitie Doa



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

Maamuzi ya Kamati Ya Maadili Baada ya Paul Makonda Kukutwa na kosa la kuingilia uhuru wa Bunge.

Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge la Tanzania, leo imewasilisha bungeni taarifa za matukio mbalimbali ambazo imezifanyika kazi ikiwa ni pamoja na kuwaita na kuwahoji wahusika kwa kukiuka kanuni za bunge nje na ndani ya bunge hilo.

Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ile ya kuingilia uhuru wa bunge kosa lililofanywa na Paul Christian Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka bungeni, viongozi hao wate wawili wamesamehewa kutokana na kukiri makosa yao na kuliomba radhi bunge la Tanzania.

Aidha, Kamati ya Maadili ya Bunge imemsamehe Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe baada ya kukiri kutoa lugha ya kudharau mamlaka ya bunge.
Pia Kamati ya Maadili ya Bunge imemuadhibu Mbunge Halima Mdee  kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyosalia kwa kudharau mamlaka ya bunge.
Hata hivyo, Bunge limeazimia kumsamehe mbunge huyo  baada ya Wabunge wa pande zote kumuombea msamaha .

Katika hatua nyingine,Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya amepewa karipio kali na Kamati ya Maadili ya Bunge kwa kosa la kudharau Mamlaka ya Spika wa Bunge.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

TUNDA Aanika Kila Kitu Juu ya Mahusiano Yake Na Young D.

VIDEO queen matata Bongo, Tunda Sebasita ‘Tunda’ hivi karibuni ameibuka na kumkana aliyewahi kuwa mpenzi wake David Ganzi ‘Young D’ kuwa si mwanaume hasa aliyewahi kutamani kuwa naye huko nyuma na juu ya uhusiano wao ni jambo ambalo lilitokea tu.
Akichonga na Uwazi Showbiz, baada ya kuulizwa ni mwanaume gani alitamani kuwa naye Bongo huko nyuma na hakupata bahati ya kuwa naye, Tunda alisema hayupo maana mwanaume aliyetamani kuwa naye amekwisha kuwanaye lakini si Young D.
“Siwezi kulitaja jina lake wazi, lakini kiukweli mwanaume ambaye nilitamani sana kuwa naye tayari nilikwishakuwanaye na tukaachana lakini naweka wazi kuwa si Young D,” alimaliza Tunda.

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

UBUYU wa Moto Moto...Kumbe Lulu Diva Ashea’ Penzi na Shangazi Yake.

Ubuyu wa kutisha! Jipu limepasuka mjini kuwa muuza nyago na msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amekiri kushirikiana ‘kushea’ penzi la bwana mmoja na shangazi yake pamoja na shosti yake wa karibu.
Kwa mujibu wa Lulu Diva, jambo hilo limekuwa likimtesa moyoni lakini kwa kuwa anataka kuwa huru, basi ameona ni vyema akalipasua.
MSIKIE LULU DIVA
“Kila mtu anapitia mambo mengi sana kwenye uhusiano wa mapenzi na maisha kwa jumla. Nimeamua kufunguka kuhusu jipu nililonalo moyoni mwangu. Ni kuhusu jamaa mmoja ambaye nilikuwa ninampenda sana katika maisha yangu.
UKIMSEMA VIBAYA…
“Kwa jinsi nilivyokuwa ninampenda yule jamaa, yaani ulikuwa ukiniambia kitu kibaya kuhusu yeye, basi ujue ni lazima nitaenda kumwambia na kukutaja. Nilikuwa sisikii wala siambiliki kwake.
AENDA KUMTAMBULISHA
“Kutokana na kudumu kwenye mapenzi kwa muda mrefu na kumuelewa, nilimuomba aje home (nyumbani) ajitambulishe ili tuwe huru, akafanya hivyo.
KUMBE ALISHA-DATE NA SHANGAZI
“Nilishangaa nilipomfi kisha pale nyumbani, watu wote wanamfahamu kama bwana’ke shangazi yangu. “Nilichoka sana kusikia vile, yule shangazi yangu, umri ni kama wangu kwa sababu tunatofautiana kama miaka minne au sita.
NDUGU WAMKATALIA
“Kutokana na hali hiyo, ndugu walikataa katakata mimi kuwa na uhusiano na mwanaume huyo kwa sababu ya kuwa na uhusiano na shangazi yangu. Familia yangu ilikataa kabisa nisiwe na uhusiano naye.
AZIBA MASIKIO
“Kiukweli nilikuwa ninampenda sana yule jamaa, niliumia, lakini nikaziba masikio na kuwaambia kuwa mimi ninampenda na siwezi kuishi bila yeye.
AVISHWA PETE
“Basi nilivyowachomolea kuachana naye, jamaa alinivisha pete ya uchumba na tukaendeleza penzi letu.
ACHEZEA KICHAPO
“Pamoja na upendo niliokuwa nao kwa jamaa, lakini bado alikuwa akinidunda sana, nilikuwa nalia, nilivumilia kwa kuhisi labda ni sehemu ya mapenzi, lakini jamaa alikuwa ananipa kichapo.
AMFUMANIA NA SHOSTI WAKE
“Nahisi jamaa alikuwa kicheche sana kwani siku moja nilimkuta anazini na rafi ki yangu, tena kwenye kitanda changu. Niliumia kwani yule rafi ki yangu alikuwa ni kila kitu kwangu, nilimuamini na kumpenda kwa dhati.
JAMAA AFUNGWA
“Baadaye yule jamaa alipata matatizo akafungwa nchini Israel, tangu kipindi hicho sijawahi kuonana wala kuwasiliana naye.
MIAKA 2 BILA KUCHEPUKA
“Kutokana na maumivu yale na misukosuko ya mapenzi, niliamua kukaa kwanza bila kujiingiza kwenye uhusiano hadi miaka miwili ilipofi ka.
HANA RAFIKI WA KIKE
“Kutokana na kile kilichotokea nikawa sina imani tena na marafi ki kwani wao wanaweza kukuharibia maisha yako, ndiyo maana mimi sina rafi ki kihivyo,” alifunguka Lulu. Lulu ambaye kwa sasa amegeukia kwenye Bongo Fleva, anatamba na Wimbo wa Malele na Usimwache.
KUTOKA KWA MHARIRI
Yapo mambo mengi mabaya na mazuri ambayo yanafanywa na watu wengi kila siku, ingawa kuna mengine yanatesa kubaki moyoni hadi pale mtu anapoamua kuyatoa na kuwa huru kama alivyofanya Lulu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

DONALD Trump Ataka Kukutana Uso Kwa Uso na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong.

Trump alisema Jumapili kwamba Kim Jong-un ni mtu mwerevu

Rais wa Marekani Donald Trump amesema angependa kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, iwapo kungekuwa na mazingira mahsusi.

Amesema ingekuwa "heshima kuu kwake".

"Kungelikuwa na hali mahsusi kwangu kukutana naye, ningekutana naye - bila shaka. Ingekuwa heshima kuu kwangu kufanya hivyo," Bw Trump aliambia shirika la habari la Bloomberg Jumatano.

Jumapili, alikuwa amemweleza Bw Kim kama "kijana mwerevu".

Tamko la Bw Trump limetokea huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Ikulu ya White House baadaye ilitoa taarifa kufafanua matamshi ya Bw Trump na kusema Korea Kaskazini ingehitaji kutimisha masharti mengi kabla ya mkutano kati ya viongozi hao wawili kufanyika.

Msemaji wa ikulu hiyo Sean Spicer alisema Washington inataka kuona tabia ya uchokozi ya Korea Kaskazini ikikoma mara moja.

"Ni wazi kwamba kwa sasa, hakuna mazingira mahsusi (ya kufanikisha mkutano kama huo)," aliongeza.

Kwenye mahojiano na CBS Jumapili, Rais Trump alisema Bw Kim alichukua mamlaka akiwa na umri mdogo, licha ya kukabiliana na "watu wagumu na hatari sana."

Alisema hajui iwapo Bw Kim ana akili timamu.

Makombora ya Korea Kaskazini

Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini aliamrisha mjomba wake auawe miaka miwili baada yake kuingia madarakani.

Aidha, anatuhumiwa kuamuru kuuawa kwa ndugu wake wa kambo.

Rais Trump, alipoulizwa maoni yake kuhusu kiongozi huyo wa Korea Kaskazini, aliambia CBS:

"Watu wanajiuliza: 'Je, ana akili timamu?' Sijui mimi...lakini alikuwa kijana wa miaka 26 au 27...pale babake alipofariki dunia. Bila shaka amekuwa akikabiliana na watu wakali na wagumu, hasa majenerali wa taifa hilo na wengine.

"Na akiwa an umri mdogo hiyo, aliweza kudhibiti madaraka. Watu wengi, nina uhakika, walijaribu kumpokonya madaraka, iwe mjomba wake au watu wengine. Na alifanikiwa kuchukua na kuyadhibiti madaraka hayo. Kwa hivyo, bila shaka, ni kijana mwerevu."

Kim Jong-un, akizuru shamba la kufugia nguruwe. Kim ameapa kuendelea kufanyia majaribio makombora

Jumamosi, Korea Kaskazini ilifanya jaribio la kurusha kombora la masafa marefu ambalo lilifeli, mara ya pili kwa jaribio kama hilo kutekelezwa na Pyongyang katika kipindi cha wiki mbili.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka siku za karibuni, huku Korea Kaskazini na Kusini zikifanya amzoezi ya kijeshi.

Marekani imetuma meli za kivita na nyambizi eneo hilo na pia imeweka mtambo wa kutungua makombora ya adui Korea Kusini, mtambo ambao maafisa wanasema umeanza kufanya kazi.

Jumapili, makala katika shirika la habari la serikali ya Korea Kusini KCNA ilitoa wito kwa Marekani kutafakari kuhusu "madhara makubwa ambayo yanaweza kusababisha na uchokozi wake wa kipumbavu wa kijeshi."

Korea Kaskazini imekuwa ikifanya majaribio ya makombora mara kwa mara miezi ya karibu na imekuwa ikitishia kufanya jaribio la silaha za nyuklia kwa mara ya sita.

Rais Trump aliambia CBS kuwa Marekani "haitakuwa na furaha sana" iwapo majaribio zaidi yatatekelezwa na Korea Kaskazini.

Alipoulizwa iwapo hili litasababisha hatua ya kijeshi kutoka kwa Marekani, alijibu: "Sijui mimi. Naam, tusubiri tuone."


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

YOUNG Dee Atoka Kivingine Chini ya Producer T Touch...Sikiliza Nyimbo yake mpya.

Msanii wa muziki wa kufoka, Young Dee ameachia wimbo wake mpya ‘Bongo Bahati Mbaya’ akiwa chini ya uongozi mpya wa producer wa Touch Sound, Mr Ttouch.


Rapa huyo aliachana na uongozi wake wa zamani, Millian Dollar Boys (MDB) baada ya kushindwa kukubaliana baadhi ya vitu na uongozi wa label hiyo.

                                          Download au Sikiliza wimbo wake mpya hapa chini. 
https://my.notjustok.com/track/download/id/212430


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
                       Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa 

ABUNGE Wamtetea Halima Mdee Asifukuzwe Vikao vya Bunge.

Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama ameongoza Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kutoa hoja ya kufanya mabadiliko ya maamuzi ya kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ambayo ilipendekeza Mbunge Halima Mdee asihudhurie vikao vyote vilivyobaki vya Bunge la Bajeti kutokana na kukutwa na kosa la kudharau mamlaka ya Spika

Waziri Mhagama amependekeza Mhe. Halima Mdee asamehewe kosa alilolifanya ila endapo atatenda kosa lingine la kudharau mamlaka ya Bunge au kuvunja kanuni za Bunge basi utekelezaji wa adhabu uanze mara moja kwa maelekezo ya kiti cha spika tena bila kuitisha kamati yoyote ya Maadili, hoja iliyoungwa mkono na wabunge wengi wa Bunge.

Baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya kamati Haki Maadili na Madaraka ya Bunge, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walitoa michango yao juu ya adhabu zilizotolewa ambapo kwa nafasi mbalimbali Wabunge kadhaa wakiwemo Mhe. Joseph Selasini, Mhe. Riziki Shangali, Mhe. Kangi Lugola, Mhe. Peter Serukamba, Mhe. Hawa Ghasia, Mhe.Abdallah Bulembo na Mhe. Janeth Mbene walisimama wakiomba Bunge kukubaliana kumsamehe Mbunge wa Kawe Halima Mdee kwani wanaamini amejifunza na kuomba kwake msamaha mbele ya Bunge ilikuwa ni ishara tosha ya kujutia kosa alilofanya.

Kwa niaba ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Almasi Maige ameunga mkono hoja ya Mhe. Halima Mdee Kusamehewa

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Monday, 1 May 2017

MBUNGE na Meya Wazuiwa Getini Ikulu Kwenda Kumuona Rais Magufuli.

Mbunge wa Moshi Mjini, Jaffar Michael na Meya wa Mji wa Moshi, Raymond Mboya wameeleza namna walivyozuiwa kuingia Ikulu ya mjini Moshi kuzungumza na Rais John Magufuli.

Viongozi hao ambao wanatokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walikumbana na kadhia hiyo jana saa 6:00 mchana wakati wakiwa katika foleni ya ukaguzi wa maofisa usalama.

Mbunge Michael alisema aliamriwa kuondoka akiwa katika foleni Ikulu, lakini akasema awali alijulishwa na Meya Mboya kuwa walihitajika katika kikao hicho. Muda huo Rais alikuwa amepanga kukutana na viongozi wa dini, alkini haieleweki ilikuwaje mbunge na meya wakaenda ikulu pasipokuwa na mwaliko.

Mbunge Michael alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo alikiri kuamriwa kuondoka akiwa katika foleni ya ikulu.


“Ni kweli nikiwa kwenye foleni alikuja ofisa usalama mmoja akaniambia kistaarabu tu kuwa mimi sikuwa natakiwa nilijaribu kumwambia mimi ni Mbunge lakini akasisitiza siruhusiwi,” alisema Mbunge huyo.

Mstahiki Meya Mboya alisema alijulishwa na viongozi wa halmashauri na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwa wangehitajika.

“Niliambiwa Mkurugenzi wangu alifanya mawasiliano na Ras (Katibu Tawala wa mkoa) na wote wakaona ipo haja ya sisi kama wenye mji kuwapo lakini ndio hivyo tulizuiwa,” alisema.

Juhudi za kuwapata maofisa wa serikali na Ikulu ndogo ya Moshi kutoa ufafanuzi zilishindikana kutokana na ama simu zao kutokupatikana na wengine kusema hawakuwepo eneo la tukio.

Chanzo: Mwananchi

Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Jiunge na group la Whatsapp la "Hebron Malele" kwa update zote habari moto,Michezo,Burudani,Makala,Video Mpya,na kudownload wimbo mpya kiulaisi.

Jiunge na group la Whatsapp la "Hebron Malele" kwa update zote habari moto,Michezo,Burudani,Makala,Video Mpya,na kudownload wimbo mpya kiulaisi Bofya hii link hapa>>>> https://chat.whatsapp.com/JKS5kYLou4uJIFPyTJDlJD


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa

MUNTARI ABAGULIWA ITALIA, MWAMUZI AMTWANGA KADI YA NJANO, YEYE AAMUA KUTOKA NJE MECHI IKIENDELEA.

Kiungo Mghana Sulley Muntari amekutana na tabia chafu na mbovu zinazopaswa kulaaniwa za baadhi ya wazungu wajinga kuamua kumbagua, jana.


Hali hiyo imemkuta katika mechi ya Ligi Kuu Italia maarufu kama Serie A wakati akiichezea Pescara dhidi ya Cagliari ambayo mashabiki wake ndiyo walimbagua Muntari ambaye baadaye alilazimika kutoka nje.
Muntari alilazimika kutoka nje baada ya kumfuata mwamuzi na kumueleza kilichokuwa kinatokea ili asimamishe mchezo kama sheria zinavyoeleza, lakini mwamuzi aligoma na kumpa kadi ya njano.


Kitendo hicho kilimuudhi zaidi na Muntari aliyewahi kung’ara na AC Milan, akaamua kutoka nje na kuiacha timu yake ikiwa na wachezaji pungufu uwanjani.
Baada ya kuona hivyo, meneja wa uwanja huo aliamua kutangaza kupitia spike za uwanja akiwaonya mashabiki hao kuacha ujinga huo.

Hii si mara ya kwanza kwa mashabiki wa Cagliari kuonyesha ubaguzi wa wazi, waliwahi kufanya hivyo kwa Samuel Et'oo mwaka 2010 wakati akiichezea Inter Milan, mwamuzi alisimamisha mchezo.
Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

PICHA:Pacha wa Lionel Messi Aonekana "Tehran" Iran.

Reza parastesh raia wa Iran anayepatikana Tehran amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya picha na muonekano wake kufanana na mwanasoka anayechezea timu ya Barcelona na Albacete Lionel Messi.
Je amefanana kweli na Messi au porojo tu



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

SERENGETI BOYS YAFANYA MAUAJI YAICHAPA CAMEROON BILA HURUMA.

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imepata ushindi wa tatu mfululizo tangu iondoke nchini kwenda kuweka kambi maalum kwa ajili ya maandalizi kujiandaa na mashindano ya AFCON kwa vijana chini ya miaka 17 itakayoanza mwezi Mei 14, 2017.

Serengeti Boys wameifunga timu ya taifa ya vijana ya Cameroon kwa goli 1-0 lililofungwa na Ally Ng’anzi kipindi cha kwanza katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Huu ni mchezo wa tatu Serengeti inashinda mfululizo, ilishinda mechi mbili za kirafiki dhidi ya Gabon zilizochezwa nchini Morocco ambako Serengeti ilikua imeweka kambi kabla ya kwenda Cameroon.

Baada ya kumaliza kambi nchini Cameroon itaondoka na kuelekea moja kwa moja Gabon ambako zitafanyika fainali za michuano hiyo ya vijana itakayoshirikisha mataifa nane.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

Lulu Diva afunguka kushea Penzi na Shangazi Yake.

Ubuyu wa kutisha! Jipu limepasuka mjini kuwa muuza nyago na msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amekiri kushirikiana ‘kushea’ penzi la bwana mmoja na shangazi yake pamoja na shosti yake wa karibu.

Kwa mujibu wa Lulu Diva, jambo hilo limekuwa likimtesa moyoni lakini kwa kuwa anataka kuwa huru, basi ameona ni vyema akalipasua.

MSIKIE LULU DIVA

“Kila mtu anapitia mambo mengi sana kwenye uhusiano wa mapenzi na maisha kwa jumla. Nimeamua kufunguka kuhusu jipu nililonalo moyoni mwangu. Ni kuhusu jamaa mmoja ambaye nilikuwa ninampenda sana katika maisha yangu.



UKIMSEMA VIBAYA…

“Kwa jinsi nilivyokuwa ninampenda yule jamaa, yaani ulikuwa ukiniambia kitu kibaya kuhusu yeye, basi ujue ni lazima nitaenda kumwambia na kukutaja. Nilikuwa sisikii wala siambiliki kwake.

AENDA KUMTAMBULISHA

“Kutokana na kudumu kwenye mapenzi kwa muda mrefu na kumuelewa, nilimuomba aje home (nyumbani) ajitambulishe ili tuwe huru, akafanya hivyo.

KUMBE ALISHA-DATE NA SHANGAZI

“Nilishangaa nilipomfi kisha pale nyumbani, watu wote wanamfahamu kama bwana’ke shangazi yangu. “Nilichoka sana kusikia vile, yule shangazi yangu, umri ni kama wangu kwa sababu tunatofautiana kama miaka minne au sita.



NDUGU WAMKATALIA

“Kutokana na hali hiyo, ndugu walikataa katakata mimi kuwa na uhusiano na mwanaume huyo kwa sababu ya kuwa na uhusiano na shangazi yangu. Familia yangu ilikataa kabisa nisiwe na uhusiano naye.

AZIBA MASIKIO

“Kiukweli nilikuwa ninampenda sana yule jamaa, niliumia, lakini nikaziba masikio na kuwaambia kuwa mimi ninampenda na siwezi kuishi bila yeye.

AVISHWA PETE

“Basi nilivyowachomolea kuachana naye, jamaa alinivisha pete ya uchumba na tukaendeleza penzi letu.

ACHEZEA KICHAPO

“Pamoja na upendo niliokuwa nao kwa jamaa, lakini bado alikuwa akinidunda sana, nilikuwa nalia, nilivumilia kwa kuhisi labda ni sehemu ya mapenzi, lakini jamaa alikuwa ananipa kichapo.

AMFUMANIA NA SHOSTI WAKE

“Nahisi jamaa alikuwa kicheche sana kwani siku moja nilimkuta anazini na rafi ki yangu, tena kwenye kitanda changu. Niliumia kwani yule rafi ki yangu alikuwa ni kila kitu kwangu, nilimuamini na kumpenda kwa dhati.

JAMAA AFUNGWA

“Baadaye yule jamaa alipata matatizo akafungwa nchini Israel, tangu kipindi hicho sijawahi kuonana wala kuwasiliana naye.

MIAKA 2 BILA KUCHEPUKA

“Kutokana na maumivu yale na misukosuko ya mapenzi, niliamua kukaa kwanza bila kujiingiza kwenye uhusiano hadi miaka miwili ilipofi ka.

HANA RAFIKI WA KIKE

“Kutokana na kile kilichotokea nikawa sina imani tena na marafi ki kwani wao wanaweza kukuharibia maisha yako, ndiyo maana mimi sina rafi ki kihivyo,” alifunguka Lulu. Lulu ambaye kwa sasa amegeukia kwenye Bongo Fleva, anatamba na Wimbo wa Malele na Usimwache.

KUTOKA KWA MHARIRI

Yapo mambo mengi mabaya na mazuri ambayo yanafanywa na watu wengi kila siku, ingawa kuna mengine yanatesa kubaki moyoni hadi pale mtu anapoamua kuyatoa na kuwa huru kama alivyofanya Lulu.


Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa

VIDEO: Hivi Ndivyo ilivyokuwa Kwenye Harusi ya Flora Kusekwa (Frola Mbasha), jijini Mwanza.

Hatimaye staa wa muziki wa Injili Tanzania Florance Henry ‘Madam Flora’ amefunga ndoa na Daudi Kusekwa baada ya kukaa muda mrefu wa upweke kutokana na kutengana na aliyekuwa mumewe Emmanuel Mbasha.



Download  Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa

                            Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
                       Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa