RAIS wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Tundu Lissu, amesema
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (Tucta) ndiye adui wa kwanza
kwa wafanyakazi.
Lissu ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema),
aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama cha
Wafanyakazi wa Nishati na Madini nchini (NUMET) katika maadhimisho ya
Siku ya Wafanyakazi Duniani mjini hapa.
Alisema Shirikisho hilo ni mwiba kwa wafanyakazi kutokana na kushindwa
kusimamia haki za wafanyafakazi kama inavyotarajiwa, badala yake
linashirikiana na Serikali kuwanyanyasa.
Kutokana na hali hiyo, Lissu aliwataka wafanyakazi kubadilika katika
mitazamo yao ili waweze kudai haki zao na siyo kuziomba kama wanavyo
fanya hivi sasa.
“Wafanyakazi badilikeni, haki haiombwi bali inatafutwa, inadaiwa hata
ukiona nchi ambazo wafanyakazi wake wanapata raha leo hii walipambana
hata kumwaga damu kwa ajili ya kupata haki zao za msingi, acheni kuwa
ombaomba wa haki zenu,” alisema.
Alisema ni vigumu kwa wafanyakazi kuomba haki zao kwa watu ambao
wamewatesa kwa zaidi ya miaka 50 kwa kuwalipa mishara midogo ambayo pia
imekuwa ikikatwa kodi kubwa.
“Wafanyakazo wadogo leo hii wanahangaika na wanahitaji unafuu maana
wanakatwa kodi ambayo hupunguza mishahara yao wakati wengine hawatoi
hata senti tano katika kodi hali hii inafanya ubaguzi wa hali ya juu,”
alisema Lissu.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa NUMET, Nicodemus Kajungu, alisema kuna
haja ya kuundwa wa shirikisho lingine la vyama vya wafanyakazi nchini
kutokana na kuonekana kuwa Tucta inawatenga.
“Leo hii sisi vyama ambavyo sio wanachama wa Tucta tumenyimwa nafasi ya
kushiriki kule Moshi, hivyo basi ipo haja ya kuwa na shirikisho letu
ambalo litasimamia kwa nguvu zote haki zetu na kuboresha maslahi ya
wafanyakazi na Tucta iendelee na wanachama wake 12 ilionao sasa,”
alisema Kajungu.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment