Siwezi kumuita Rais wetu Mh. J.P Magufuli kama Dikteta au mwenye Ukatili
na asiyewajali watu wake ila kuna kauli zake zimekuwa zikisababisha
mateso makubwa sana kwa wananchi wake.
Ukiacha zile za wakati wa Njaa na Tetemeko la ardhi.
Mfano mkubwa mzuri ni hili neno alilotoa kuhusu ukataji wa umeme kuwa
endapo mwananchi yeyote wa mahali popote atakuwa/watakuwa hawajalipia
umeme basi TANESCO wasihoji chochote bali wakate umeme.
Amekuwa akisema kuwa hata kama ni Ikulu haijalipia umeme (kitu ambacho
kamwe hakiwezekani) basi wakate ilihali umeme haukatiki huko asilani.
KINACHOUMIZA ZAIDI, leo Mbunge wa Morogoro kupitia CHADEMA ameelezea
hali inayosikitisha na kuhuzunisha sana kuwa Wafungwa (Wanaume, Wanawake
na Watoto) wa magereza ZOTE za mkoani morogoro wanaishi katika giza
tororo kisa Umeme umekatwa huko.
Hali hiyo imekuwa ikisababisha hata wafungwa watoto kubakwa na kulawitiwa, wanawake kubakwa na kupata mimba kiholela.
Na isitoshe mazingira ya magereza ni magumu sanaa kwa binadamu yeyote kuishi.
Hivi sio serikali inayopaswa kulipia umeme wa magereza? Au ni hao wafungwa?
Ni kwanini Mh. Rais asifute hii kauli yake kwa sehemu kama hizi?
Je wananchi wa maeneo haya wanamchukuliaje Mh. Rais?
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment