Msanii wa muziki wa bongo fleva, Afande Sele amefunguka na kusema kama
angekuwa ni mmoja kati ya Rais wa awamu ya tatu au awamu ya nne basi
angekaa kimya na kujifungia ndani huku akitubu na kuwaomba radhi
wananchi kwa mambo waliofanya.
Afande Sele ambaye pia ni mwanasiasa aliyegombea ubunge jimbo la
Morogoro Mjini kupitia ACT Wazalendo, amesema hayo siku moja baada ya
Rais John Pombe Magufuli kupokea ripoti ya uchunguzi wa madini ambayo
imeonyesha kulikuwa na wizi mkubwa jambo lililopelekea Rais kumtengua
Prof. Muhongo katika nafasi yake ya Waziri wa Nishati na Madini.
"Baada ya kupata matokeo ya taarifa ya tume iliyoundwa na Rais Magufuli
kuhusu usitishwaji wa kusafirisha mchanga wa madini kwenda nje ya nchi.
Nimechoka mwili na akili kwa jinsi kama taifa lenye mamilioni ya watu
masikini sana tulivyokuwa tunapoteza mabilioni ya dolla kikatili kabisa
kwa makusudi ya watanzania wenzetu wachache tena wale tuliokua tumewapa
dhamana kuu za kutuongoza." alisema Afande Sele
Afande Sele alizidi kusisitiza kuwa viongozi hao wanapaswa kuomba radhi
kwa wananchi kwa madudu ambayo wamefanya kipindi cha utawala wao
"Kwa sababu uso umeumbwa na haya na kwa sababu mimi siyo mwanahizaya.
Laiti kama mimi ningekua ni mmoja kati ya watu hawa daima ningefunga
mdomo wangu, ningejifungia ndani kwangu, ningetubu kwa Mungu wangu,
ningewaomba msamaha wananchi wenzangu kwani wametia aibu wanapaswa
kutubu" alisema Afande Sele
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment