Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwingulu Nchemba amewachana wanasheria
wakuu wa Serikali wastaafu kwa kuwataka waeleze hadharani maslahi
walionayo kwenye kampuni za madini zinazosafirisha mchanga nje ya nchi.
Wanasheria hao wakuu wa serikali wastaafu, ni Andrew Chenge na Jaji
Frederick Werema na amewataka wamwache Rais John Magufuli aendelee
kulinda rasilimali za umma, zisiliwe na watu wachache.
Mwingulu amesema hayo juzi wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara
uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa Tarafa ya Ndago, jimbo la Iramba.
Alisema Chenge na Werema kwa nyakati tofauti wakiwa wanasheria wakuu wa
Serikali, pamoja na majukumu yao mengine, wameshiriki kusaini mikataba
mikubwa mikubwa, ikiwemo ya makampuni ya kuchimba madini.
“Kwa akili ya kawaida tu, baadhi ya mikataba mikubwa ikiwemo ya
makampuni ya madini, haikuwa sawa… Ndio maana imelalamikiwa kwa muda
mrefu,” alifafanua Mwigulu.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment