Mbunge Nape Nnauye ljana bungeni wakati akichangia katika bajeti
ya Wizara wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji amesema Wanakusini
hawatakubali kuona ujenzi wa kiwanda cha mbolea Lindi unakwama kutokana
na vita iliyopo kati ya mataifa makubwa.
Nape Nnauye amemtaka Waziri Mwijage asikubali kuona vita ya mataifa
hayo inaendelea kuwaumiza wananchi wa Kusini na kusema kama atafanya
hivyo wao hawatakubali hilo jambo.
“Mwijage viwanda ni ukombozi hasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara
kwa sababu bado ni masikini sana na ukombozi wowote una vita, hasa kwa
wale ambao wanafaidika na mfumo wa kutokuwepo kwa viwanda.
Na hapa
nitatoa mfano. Tumekuwa tukizungumza juu ya ujenzi wa kiwanda cha mbolea
Lindi, Kilwa pale ila taarifa tulizonazo mataifa makubwa yenye
‘interest’ na mbolea katika nchi hii yanapambana kuhakikisha
kiwanda
hicho hakijengwi. Katika jambo ambalo hatutakubaliana nalo Mwijage ni
pamoja na hili, kuruhusu vita hii iendelee kutuumiza wanakusini” alisema
Nape Nnauye
Nape Nnauye aliendelea kusisitiza
“Mataifa hayo yanapigana kwa maslahi yao na kama serikali mtayumba
kwenye hili basi Wanakusini hatutokubali, tulishalizungumza,
mlishakubaliana, mwekezaji alishapatikana na utaratibu uko wazi, sasa
vita hii ya wakubwa isituumize sisi wakapiganie nje ya Lindi lakini
tunakitaka kiwanda cha mbolea Lindi” alikazia Nape Nnauye
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment