Rais John Magufuli leo (Jumamosi) amemkabidhi rasmi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kwa Rais Yoweri Museveni.
Muda mfupi kabla ya kumkabidhi nafasi hiyo, Rais Magufuli ambaye alikuwa
mwenyekiti wa EAC kwa miaka miwili amewashukuru wanachama wa jumuiya
hiyo kwa kumuamini na kumpa nafasi hiyo miezi michache baada ya kuingia
madarakani.
“Mliniamini mkanichagua licha ya kuwa madarakani kwa muda mfupi,”amesema
Rais Magufuli ambaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa EAC, mapema mwaka
jana.
Rais Magufuli amesema anaimani na Rais Museveni kuwa atafanya kazi nzuri kutokana na uzoefu wake.
“Yaliyonishinda kuyatatua, atayatatua yeye (Rais Museveni),”amesema.
Mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo, Rais Museveni ambaye sasa ni
mwenyekiti wa EAC amesema atahakikisha anatumikia nafasi hiyo kwa nguvu
na uwezo wake wote.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment