Mbunge wa Mtama, Nape Moses Nnauye amemjia juu kwa mara nyingine Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam kwa kusema kwamba hakuunda kamati ya kumchunguza
yeye, bali aliunda kamati ya kuchunguza tukio la kuvamiwa kwa kituo cha
utangazaji cha Clouds Media Group.
Nape ameyasema hayo mapema leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa Twitter,
ambapo alieleza kwamba, kama kiongozi huyo alikuwa ni mmoja wa wavamizi
wa kituo hicho, basi hayupo juu ya sheria.
“Niliunda kamati kuchunguza tukio la kuvamiwa kituo cha utangazaji sio
kumchunguza RC. Kama RC alikuwa mmoja wa wavamizi, hayuko juu ya
sheria,” aliandika Nape
Alipoulizwa kwanini Waziri wa Habari aunde kamati ya uchunguzi wa tukio
la uvamizi badala ya kamati hiyo kuundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Nape alijibu kwa kuuliza swali kama kila kamati inaundwa na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Majibu haya ya Nape yamekuja ikiwa ni saa chache baada ya kuulizwa ni
yapi maoni yake kuhusu kauli ya Makonda kwamba hakuwa akifahamu mipaka
yake ya kazi ndio sababu alikwenda kuunda tume ya kumchunguza.
Kauli ya Nape kuhusu kuunda kamati imekuja ikiwa ni takribani saa 24
tangu Makonda aliposema kuwa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo aliunda kamati ya kumchunguza.
Makonda alisema hayo jana, ambapo alidai kuwa kamati iliyoundwa na
Waziri isingeweza kumhoji kwa sababu haikuwa na uwezo huo kutokana na
wajumbe wa kamati hiyo kutofahamu mambo yanayohusiana na masuala ya
uvamizi.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment