Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amefunguka na
kusema Watanzania tumerogwa kwani tuna kila kitu ambacho kinaweza
kutufanya kuwa mbele kimaendeleo lakini siku zote tumekuwa nyuma.
Mchungaji Gwajima amesema hayo leo wakati akitoa mahubiri yake
kwenye kanisa lake na kusema Watanzania wamerogwa kwani wanapenda sana
maandamano na vitu visivyo na msingi kuliko kufanya kazi, anasema
Tanzania ina vitu na mali nyingi
“Ukitaka kuingoza Tanzania lazima uwe na moyo wa mwendawazimu
maana watu wake wamerogwa mpaka wamerogeka, ni nchi ya waliorogeka tu
unaweza kwenda kusaini mikataba ya madini, nenda kasaini mkataba wa
madini Japan au Kenya uone, sisi Tanzania Watanzania tunauza ubuyu na
karanga mzungu anabeba kila kitu, sisi tumerogwa. Tanzania ina mito
mingi yenye maji lakini maji yanakwenda tu, watu hawalimi” alisema Gwajima
Mbali na hilo Gwajima amempa tano Rais Magufuli kwa kitendo chake
cha kuzuia makontena ya madini na kusema ni hatua nzuri na Rais
ashikirie hapo hapo
“Hata kama tulisaini mikataba ya kufa mtu sawa tu Rais ashikirie
hapo hapo hakuna kuruhusu makontena mpaka wazungu macho yao yawe
mekundu, kama hatujawa tayari kuchimba madini tuyaache kwanza, wapo
wanaosema sijui tutashitakiwa, sijui mikataba itatubana ondoka na
makaratasi yako hapa yale madini ni ya kwetu, mwanasiasa unayetaka kulia
ulie tu na ufe madini hakuna kwenda” alisema Gwajima
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment