Watu wawili wanaodhaniwa ni wapenzi, wameuawa kwa kuchomwa moto
baada ya kufungwa kamba wakiwa kitandani, katika tukio lililotokea eneo
la Whiterose lililoko kata ya Kiranyi wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Mamia ya watu wamejitokeza kuzunguka nyumba lilipotokea tukio hilo
baada ya kuona moshi ukitoka katika moja ya chumba na kuonekana miili
ikiwa imeteketea kwa moto.
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo amesema tuki hilo limetoke jana, Jumanne saa 3.00 asubuhi
Amesema aliyekutwa amefariki ni Maurine Urio (32) pamoja na
rafiki yake huyo ambaye hajaweza kutambulika kutokana na kuungua sana.
“Tumepata taarifa asubuhi hii kuwa kuna nyumba inaungua na
polisi pamoja na zimamoto walifika eneo la tukio na kukuta watu hao
wameshapoteza maisha wakiwa juu ya godoro ambako mwanaume alionekana
kabla ya kuchomwa alifungwa kamba miguu na mikono ili kuzibitiwa,”amesema.
Mkumbo amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha
kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa Mount Meru huku wahusika wa
tukio hilo wakiwa wanatafutwa.
Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Ilkiurei iliyoko kata
ya Kiranyi, Onesphory Chami amedai kuwa tukio hilo linahusishwa na wivu
wa mapenzi.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment