Msanii wa hip hop, Kala Jeremiah amemuomba Waziri Mwakyembe kutengua
kauli yake ya kuwataka wasanii waache kuimba nyimbo zinazohusu siasa,
kwa madai kuwa ni kuwatenga mbali na jamii inayotegemea wasanii
kuwasemea mahitaji yao.
Akizungumza kwenye 'story' tatu ndani ya Planet Bongo, Kala amesema kuwa
kauli ya Mh. Mwakyembe haiko sawa kwani inatengeneza 'gap' kubwa kati
ya jamii na wasanii na kuongeza kwamba siasa zinazoimbwa na wasanii
ndizo ambazo zinasaidia jamii na wakati mwingine zinasaidia serikali
kutopoteza pesa.
Aidha Kala amendelea kufunguka kwamba yeye kama msanii anayeimba
harakati kwa ajili ya kusaidia jamii yake kauli ya Waziri ni kama
inamlazimisha kuimba nyimbo za mapenzi kitu ambacho kwake hakitampa
tatizo lakini hasara itakuwa kwa jamii inayohitaji kusemewa.
Pamoja na hayo Kala amefunguka na kusema wimbo wake alioimba kuwasemea
watoto yatima 'Wanandoto' umempatia sifa kubwa kutoka kwenye mashirika
mbalimbali yanayojihusisha na kusaidia watu wenye matatizo na kumpongeza
kwa kuweza kufikisha ujumbe mzito pasipo kutumia gharama kubwa sana.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment