Watumishi zaidi ya sabini wamesimamishwa kazi wilayani Misungwi
Mwanza kwa kukutwa na vyeti feki, ubadhilifu wa mali za Umma na utovu wa
nidhamu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi Bw. Athon Masele amesema kuwa
watumishi 68 wamekutwa na vyeti feki, wawili walikuwa ni wabadhilifu wa
mali za Umma huku wengine wawili walikuwa ni watovu wa nidhamu, jambo
ambali limepelekea idara ya elimu na afya kuathirika kwa kiwango kikubwa
zaidi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mh. Charles Kitwanga
amesema mwaka jana walisimamishwa kazi watumishi wawili kwa tuhuma za
ubadhilifu wa mali za umma ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja mapato
yameongezeka kwa kiwango kikubwa kutoka kiasi cha shilingi milioni 24
hadi shilingi milioni 120 kwa mwezi hali iliyosaidia kupata hati safi
baada ya CAG kuridhishwa na utendaji kazi wa halmashauri
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza HapaFollow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment