Kamati ya Saa 72 imekaa kupitia mambo mbalimbali na moja ya uamuzi wake ni kuhusiana na Yanga kugoma kuingia vyumbani.
Mechi namba 231 (Yanga 2 Vs Mbeya City 1).
Timu zote mbili hazikupita kwenye mlango
rasmi wakati wa kuingia uwanjani katika mechi hiyo iliyochezwa Mei 13,
2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Hivyo, kila klabu imepigwa
faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kitendo hicho, uamuzi ambao
umezingatia Kanuni ya 14(48).
Washabiki wa Yanga walivunja uzio wa
ndani (fence) wa upande wa Magharibi wakati wakiingia uwanjani
kusherehekea ubingwa wa timu hiyo. Hivyo, klabu ya Yanga imeagizwa
kulipa gharama za uharibifu huo uliofanywa na washabiki wake, uamuzi
ambao umezingatia Kanuni ya 42(3) ya Ligi Kuu.
Pia Yanga imepigwa faini ya sh.
1,500,000 (milioni moja na laki tano) kwa kutoingia vyumbani. Adhabu
hiyo imezingatia Kanuni ya 14(8) ya Ligi Kuu. Vilevile klabu hiyo
imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na kuonyesha vitendo
vinavyoashiria ushirikiana. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni
ya 42(1) ya Ligi Kuu.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment