Baada ya mahojiano ya jana ya mtu kukwepa kuzungumzia suala la kufoji
vyeti vya elimu, kuna watu wanaliona hili ni jambo dogo, hivyo
kujitokeza kule, kumelimaliza rasmi, no its not over until it is over!.
Japo kwa mujibu wa katiba yetu, rais wa JMT ndio mamlaka kuu kupita
zote, lakini sii wengi wanaotambua kuwa mamlaka ya juu kabisa ni katiba
ya JMT, na rais wa JMT, japo amejiweka juu ya katiba, lakini kiukweli
yuko chini ya katiba, hivyo hili suala la mteuliwa Daudi Bashite, watu
wanalichukulia kimzaha mzaha au kiutani utani, lakini tungekuwa ni nchi
nyingine yenye watu wanaojielewa, jee unajua suala kama hili lingeweza
kabisa kumng'oa rais Magufuli pale Ikulu kwa mujibu wa sheria akaondoka
na Bashite wake?.
Tanzania ni nchi inayoongozwa na Katiba kwa mujibu wa sheria, taratibu
na kanuni. Ikithibika beyond reasonable doubt kuwa Daudi Albert Bashite
ni kweli alifeli kisha akafoji vyeti na kufoji jina, kujiendeleza
kielimu hadi kuteuliwa, then huyu ni muhalifu kama wahalifu wengine
wote, then hata rais wa JMT ampende vipi, anaweza kulazimishwa kutengua
uteuzi wake kwa kuamrishwa, na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, na
rais asipofanya hivyo, then rais anaweza kushitakiwa na Bunge na
kuondolewa madarakani!.
Watanzania tumekuwa ni watu wa kupiga sana kelele, kulaumu, kulalamika,
kushutumu bila kuchukua hatua zozote ili hali sharia zipo lakini
hatuzitumii.
Sakata la Bashite ni jambo dogo sana kulishughulikia kisheria.
Hatua za kufuata.
1. Any interested party mwenye ushahidi usio shaka kuwa Daudi Albert
Bashite ni muhalifu wa kufoji vyeti na kuiba jina, kupitia kwa
mwanasheria binafsi anaweza kufungwa mashitaka ya kijinai dhidi ya Daudi
Albert Bashite as a private investigations. Atapewa vibali vyote toka
ofisi ya DPP. Kuanzisha uchunguzi.
2. Uchunguzi utaanzia kwa Daudi Bashite mwenyewe kuitwa kwa samansi ya
kuhojiwa kijinai chini ya kiapo. Na akikiri tuhuma, suala la uchunguzi
wa kijinai unaishia hapa, mtuhumiwa anaandika barua ya kujiuzulu na
issue hii inamalizika rasmi.
3.Kwenye mahojiano hayo kama atakanusha kuwa yeye si Daudi Bashite kama
alivyodanganya jana pale Star TV, then kazi ya kukusanya ushahidi
inaanza kwa kutolewa samansi ya kuwahoji wahusika wote wakuu isipokuwa
mke, mzazi, walimu, hospitali kufuatia kitu kinachoitwa "fiduciary
relationship" ambapo sheria inampa kinga ya kuhojiwa kijinai mtu wa
karibu kama mke dhidi ya mume, mzazi na mtoto, mwalimu na mwanafunzi,
daktari na mgonjwa, mwanasheria na mteja, padri na muumini etc. Hivyo
kuanzia hospitali aliyozaliwa utakusanywa ushahidi wa documentary
evidence aliandikishwa kwa majina gani?. Kisha Vizazi na Vifo kupata
cheti cha kuzaliwa. Shule alipoandikishwa darasa la kwanza. Shule ya
sekondari, Necta, vyuo, ajira alipitia, hadi idara ya uhamiaji.
4. Baada ya kukamulisha kukusanya documentary evidence, usio tia shaka
kuwa Daudi Bashite amefoji vyeti. Then linafunguliwa shauri lunaloitwa
"quo warranto" kuwa rais amemteua muhalifu, hivyo mahakama inajiridhisha
na ushahidi uliiowasilishwa mbele yake.
5. Ndipo mahakama inatoa hati ya Quo Warranto kumlazimisha rais wa JMT,
atake asitake, kutengua uteuzi wa Daudi Bashite kwa makosa ya uhalifu wa
kijinai. Kwa mujibu wa katiba yetu, rais wa JMT, hana mamlaka ya
kumteua muhalifu kwenye utumishi wa umma.
6. Kama rais atetengua uteuzi huu, then DPP atakuwa huru kumpandisha
kizimbani Daudi Bashite kujibu tuhuma za jinai zinazomkabili na
kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria.
6. Iwapo Rais wa JMT asipotekeleza amri halali ya mahakama, anakuwa
amepoteza sifa za urais zilizoainishwa na katiba ya JMT ya mwaka 1977.
Hivyo rais anashitakiwa bungeni na kuondolewa kwenye urais kupitia
process ya impeachment.
NB.
7. Process nilizoziweka hapo ni kwa mujibu wa katiba, sasa suala kama
mahakama zetu zina weza kutoa amri ya Quo Warranto au laa linabaki
kwenye utelelezaji, kitu cha muhimu ni kuelimishana kuwa rais wa JMT sio
kila kitu, katiba ndio kila kitu. Maadam sheria zipo, suala la sheria
kufuatwa au kutofuatwa hili sio langu.
8. The same applies to impeachment process, kuna watu wanadhani mtu
akiishachaguliwa kuwa rais wa JMT, anaweza kujifanyia lolote analotaka,
no! . Urais wa JMT ni kwa mujibu wa katiba, rais wetu atatekeleza
majukumu yake ya urais kwa mujibu wa katiba, na ili kumkinga
asibuguthiwe, ndio maana katiba yetu imempa kinga ya kutokushitakiwa
mahakamani, lakini hakuna kinga ya kutokushitakiwa na Bunge pale
anaposhindwa majukumu yake ya urais ikiwemo kututeulia wahalifu wa
makosa ya jinai if proved beyond reasonable doubt, rais anashitakiwa na
Bunge na anang'olewa na kuondoka na Bashite wake. Sasa suala la Bunge
letu kama linauwezo wa kufanya hivi au laa, hili sio langu ni la wabunge
wenyewe. Kitu cha muhimu hapa ni kujua kuwa hata rais anaweza
kung'olewa madarakani na Bunge.
9. Hili sio lazima lifanywe na sheria, hata sisi media tunaweza, tukiwa
na strong media yenye uzalendo usiatia shaka yenye kujua wajibu wake kwa
umma, unaweza kuchunguza ukweli wa tuhuma hizi na kuziripoti, hivyo ama
kumlazimisha rais wa JMT atimize wajibu wake, au kile kiti akione
kichungu na kuachia kwa aibu kama ilivyowahi kutokea nchini Marekani kwa
rais Richard Nikson kuachia ngazi kwenye kashfa ya Watergate.
10. Nawahakikishia hata mimi mwenyewe tuu kupitia kampuni yangu ya PPR,
hili naliweza kabisa, ila kwa bahati mbaya sana, siwezi kulifanya kwa
sababu kampuni yangu ya PPR, imejikita kwenye habari za kimaendeleo tuu
zenye maslahi kwa taifa, yaani developmental news za Tanzania hapa
tulipo, tufanyeje ili tufike kule tulikopaswa na sio habari kama hizi za
vyeti vya Bashite.
Jumanne Njema.
Paskali
Chanzo - Jf
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment