Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole
amesema kuwa ni ruksa kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA)
kutumia ukumbi wao wa mikutano maarufu kama 'Dodoma Convention Centre'.
Kauli hiyo imetolewa na Polepole kufuatia mazungumzo aliyofanya kwa njia
ya simu na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe tarehe 14 Mei
2017 juu ya uwezekano wa chama hicho kutumia ukumbi huo. Polepole
amemwambia Mbowe kuwa CCM haioni uzito wa kutoa kibali kwa CHADEMA
kutumia ukumbi huo ikiwa watawasilisha maombi rasmi kwa Katibu Mkuu
Abdulrahman Kinana.
Hata hivyo, Polepole amemweleza Mbowe kuwa wataruhusiwa tu kuutumia
ukumbi huo ikiwa watakubali masharti ya kutoweka alama za chama chao nje
ya ukumbi huo isipokuwa sehemu ya ndani.
Tarehe 27 Mei 2017, CHADEMA watafanya Mkutano wa Kamati Kuu Mjini Dodoma
na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa chama hicho Boniface Makene
haijabainisha ukumbi watakaotumka. Upo uwezekano kuwa Mbowe ametekeleza
masharti aliyopewa na huenda mkutano huo utafanyika ndani ya ukumbi wa
CCM.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment