Watoto
watatu walionusurika katika ajali basi iliyosababisha vifo vya
wanafunzi, walimu pamoja na dereva wake mjini Arusha wanatarajiwa
kusafirishwa kwenda kupatiwa matibabu zaidi nchini Charlotte North
Carolina mwishoni mwa juma hili.
Mwinjilisti
maarufu duniani kutoka Shirika la Samaritan Purse, Bill Graham wa
Marekani ndiye aliyebeba gharama za kukodisha ndege maalumu aina ya DC 8
kupeleka wanafunzi waliojeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea mwishoni
mwa wiki iliyopita wilayani Karatu, Arusha.
Watoto hao wameumia shingo, miguu na sehemu mbalimbali za miili yao.
Kwa
mujibu wa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyarandu
aliyezungumza jana na waandishi wa habari mjini Arusha, gharama za
kukodisha ndege kwenda Marekani si chini ya dola za Kimarekani 350,000
(Sh milioni 700). Gharama hizo ni nje ya matibabu, chakula na malazi kwa
wakati wote ambao wagonjwa hao na wasindikizaji watakuwa nchini humo.
“Tumefanikiwa
kupata ndege aina ya DC 8 kutoka Shirika la Samaritan Purse
linaloongozwa na mtoto wa Billy Graham aitwaye Franklin kwa ajili ya
kuwasafirisha watoto Doreen Mshana, Sadia Awadh na Wilson Tarimo na
wazazi wao watatu, yaani mama zao,” alisema Nyalandu akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Alisema
pia watoto hao wataambatana na daktari wa hospitali ya mkoa wa Arusha
ya Mount Meru, Elias Mashalla na muuguzi Simphorosa Silalye.
Kwa
mujibu wa Nyalandu, ndege hiyo inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kilimanjaro KIA) leo jioni ikitokea Charlotte ,Jimbo la
North Carolina, Marekani.
“Endapo
taratibu za safari ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa visa utafanikiwa,
basi ndege inaondoka na wagfonjwa na wasindikizaji Jumapili (kesho) na
baada ya kufika mjini Charlotte, North Carolina watasafiri kwa ndege
nyingine maalumu ya kubeba wagonjwa hadi mji wa Sioux City, Iowa ambako
watapokelewa na uongozi wa Hospitali ya Mercu na Shirika la STEMM,” alisema Nyalandu.
Alitumia
fursa hiyo kuwataka Watanzania kupongeza juhudi za Rais, Dk John
Magufuli, Makamu wake, Samia Suluhu Hassan na uongozi wa Mkoa wa Arusha
chini ya Mkuu wa Mkoa, Mrisho Gambo kwa kuguswa na kushiriki katika kila
hatua kuanzia baada ya ajali, mazishi hadi ufuatiliaji wa afya za
majeruhi.
‘’Hili
jambo ni letu sote hapa, hatuhitaji sifa bali tunachopaswa Watanzania
wote kushirikiana kwa pamoja na kuweka mbele ubinadamu na kujitoa kwa
hali na mali kuwasaidia hawa watoto ili waweze kupata nafuu na kurudi
shuleni,” alisema
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gambo alisema kuwa katika michango yote
iliyochangwa kwa ajili ya rambirambi kwa msiba huo mpaka jana
zilipatikana fedha kiasi cha Sh milioni 215.
Gambo
alisema katika fedha hizo, kila familia ilikabidhiwa zaidi ya Sh
milioni 3.8 na pia Serikali ilibeba gharama za usafiri, majeneza, mafuta
ya magari na malipo ya madereva.
Alisema Sh milioni 190 zilitumika katika matumizi mbalimbali ya msiba huo na kuwataka walioahidi kuchangia kutimiza ahadi zao.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment