Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeitupilia mbali maombi yaliyofunguliwa
na Bodi ya wadhamini ya CUF dhidi ya Mbunge wa Kaliua, Magdalena
Sakaya(CUF), Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma(CUF) na wenzao sita
yakuomba mahakama iwazuie kwa muda kujihusisha katika masuala ya uongozi
na kufanya mikutano ya chama.
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa uamuzi huo baada ya kusikiliza pande zote mbili.
Hakimu Mashauri amesema Joram Bashange ambaye aliapa katika kiapo kuwa
ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya CUF aliapa uongo kwa sababu bodi hiyo
ilikwisha muda wake.
Hivyo, Bashange kuwa ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya CUF ni uongo na kwamba yeye binafsi atabeba gharama za kesi.
Katika kesi hiyo Sakaya na wenzake walikuwa wakiwakilishwa na Wakili,
Mashaka Ngole huku bodi ya wadhamini ya CUF ikiwakilishwa na Wakili
Hashimu Mziray.
Download Application ya Hebron Malele Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi>>>>Bonyeza Hapa
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment