Watoto watatu wa shule ya msingi ya Lucky Vicent walionusurika
katika ajali ya basi, wamefanyiwa upasuaji na sasa wapo wodini
wakiendelea na mazoeazi, ila Doreen, jana alipewa MAPUMZIKO maalumu
akiwa anaandaliwa tayari kwa UPASUAJI wa uti wa mgongo ‘spine’
unaofanyika leo.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliyeshiriki katika
kuwasafirisha watoto hao, ameandika katika ukurasa wake wa facebook
akisema watoto hao kwa sasa wamewekwa kwenye vyumba vya peke yao.
Upasuaji huo umefanyika katika Hospitali ya Mercy, Sioux City, Marekani.
Amefafanua upasuaji waliofanyiwa na kusema mtoto Saidia alifanyiwa
upasuaji wa mfupa wa kulia wa nyonga, mkono wa kulia na kuwekewa ngao
kwenye shingo atakayotakiwa kukaa nayo kwa wiki sita.
“Kwa upande wa mtoto Wilson, yeye amefanyiwa upasuaji wa nyonga ya
kulia, kiwiko cha kulia kilichokuwa kimevunjika mara tatu na kiwiko cha
kushoto,” amesema
Follow me instagram>>>Bonyeza Hapa
Facebook page like hapa>>>Bonyeza Hapa
Jiunge na group la whatsapp>>>Bonyeza Hapa
0 comments:
Post a Comment